The House of Favourite Newspapers

Simba Yampiga 8-0 Singida Uwanja wa Uhuru, Kagere Atupia Nne

0

Mshambuliaji Meddie Kagere amefunga mabao manne wakati Simba ikichakaza timu dhaifu ya Singida United kwa mabao 8-0 kwenye Uhuru, Dar es Salaam.

 

Simba imetoa kipigo hicho kizito kwa vibonde wa ligi Singida United wakiwa pungufu ikiwa ni siku nne tu tangu walipofungwa na watani zao wa jadi Yanga kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 71, kileleni huku mshambuliaji Kagere akifikisha mabao 19 na sasa anahitaji magoli manne kufikia rekodi yake ya msimu uliopita ya magoli 23.

Vikosi

Simba: Aishi Manila, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Tairone Santos, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Deo Kanda, Luis Miquissone, Meddie Kagere, John Bocco na Hassan Dilunga.

 

Singida United: Owen Chaima, George Wawa, Haji Mwinyi, Meshack Kibona, Tumba Swedi, Cleophace Sospeter, George Sangija, Haruna Moshi ‘Boban’, Steven Sey, Seiri Arigumaho na Mtikila Hussein.

Leave A Reply