The House of Favourite Newspapers

Simba yaongoza Ligi Kuu Bara, Simba 2, Mbeya City 0

0

Lyanga (9)

Mfungaji wa bao la kwanza la Simba, Danny Lyanga.

IMG_6986

Mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza akidhibitiwa na mabeki wa Mbeya City.

MABAO mawili yaliyofungwa na Danny Lyanga na Ibrahim Ajib katika dakika ya 75 na 90 yameipa Simba ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Danny Lyanga
Simba imepata ushindi katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ambapo sasa imeshika usukani wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 48 ikiizidi Yanga ambayo ina pointi 47 sawa na Azam inayoshika nafasi ya tatu.

Ushindi huo ulisababisha shangwe nyingi kwa mashabiki wa Simba ambao waliondoka uwanjani hapo wakiwa na furaha huku wakishangilia barabarani.

Mara baada ya mchezo huo, Kocha wa Simba, Jackson Mayanja alisema anashukuru mashabiki wa timu yake kwa kuendelea kuiunga mkono timu yao huku akipongeza wachezaji wake kwa kuifunga Mbeya City kwa mara ya kwanza katika uwanja huo.

Upande wa Mbeya Ciy, Kinnah Phiri alisema kilichotokea ni timu yake kukosa bahati tu lakini vijana wake walicheza vizuri. Kingine alisema wachezaji wake walikuwa wakipata nafasi ya kupiga mashuti lakini hawakufanya hivyo, ameahidi kwenda kulifanyia kazi suala hilo.

Kikosi cha Simba:

  1. Vincent Angban
  2. Emiry Nimubona
  3. Mohamed Hussein ‘Tshabalala’
  4. Novaty Lufunga
  5. Juuko Murshid
  6. Justice Majabvi
  7. Mwinyi Kazimoto
  8. Jonas Mkude
  9. Hamis Kiiza
  10. Ibrahim Ajib
  11. Brian Majwega

Kikosi cha Mbeya City

  1. Hannington Kalyesebula
  2. Hassan Mwasapili
  3. Abubakar Shaban
  4. Tumba Sued
  5. Haruna Shamte
  6. Kenny Ally
  7. Raphael Alpha
  8. Haruna Moshi ‘Boban’
  9. Geofrey Mlawa
  10. Joseph Mahundi
  11. Ditram Nchimbi
Leave A Reply