The House of Favourite Newspapers

Simba Yapangua Ratiba ya Yanga, Wiki ya Mwananchi

0

UELEKEA mchezo wa Ngao ya Jamii utakaozikutanisha Simba na Namungo utakaopigwa Agosti 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, imefanya kusogezwa mbele kwa ratiba ya mechi ya kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Aigle Noir ya Burundi.

 

Yanga na Aigle Noir ambao watacheza Uwanja wa Mkapa jijini Dar kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi, mechi yao awali ilipangwa kuanza saa 10:00 jioni, lakini imesogezwa mbele hadi saa 1:00 usiku.

Ile ya Simba vs Namungo, itaanza saa 9:30 alasiri.Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amesema: “Mchezo wetu dhidi ya Aigle Noir uliopangwa kuchezwa saa 10:00 jioni tumeusogeza mbele hadi saa 1:00 kutokana kuupa heshima mchezo wa Ngao ya Jamii ambao unaashiria ufunguzi rasmi wa msimu wa 2020/21, hivyo basi tunaangalia utaratibu wa kusogeza ratiba yetu kuona mashabiki wetu wanaendelea kupata burudani za kutosha wakati wakisubiri mechi.

”Katika kilele cha Wiki ya Mwanchi, Yanga mbali na kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Aigle Noir kutoka Burundi, itatambulisha kikosi chake kitakachoshiriki msimu wa 2020/21.

STORI: HUSSEIN MSOLEKA , Dar es Salaam

STEVE NYERERE Amuonya WEMA kuhusu CARLINHOS – “TUNAKUJUA MLEZI wa WANA, TUTAKUPIGA”

Leave A Reply