The House of Favourite Newspapers

Simba Yapata ushindi wa Bao 4-0 Dhidi ya Tabora United

0

Magoli kutoka kwa Pa Omary Job, Sadio Kanouté, Che Fondoh Malone na Fred Michael yameiwezesha Klabu ya Simba kupata ushindi huo dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora

Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha pointi 29 ikiendelea kubaki nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Ligi ikiwa imecheza mechi 12, huku Yanga ikiongoza kwa kuwa na pointi 34 katika michezo 13, ikifuatiwa na Azam FC pointi 31 mechi 13

Mchezo ujao wa Simba utakuwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba (Mwanza), dhidi ya AzamFC mnamo Februari 9, 2024 wakati Tabora United imebaki katika nafasi ya 12 kwenye msimamo ikiwa na pointi 15 katika michezo 14

Leave A Reply