Simba Yapewa Onyo Kali Kwa UD Songo

ALIYEWAHI kuwa straika wa Simba na sasa anaichezea Royal Eagles ya Afrika Kusini, Uhuru Selemani amefunguka kuwa Simba inapaswa kuwa makini na UD Songo kwa sababu ni timu ambayo huwa makini zaidi inapokuwa kwao.

 

Uhuru aliwahi kuitumia Klabu ya UD Songo mwaka 2017 na ilifanikiwa kuutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Msumbiji. Simba inatarajiwa kuvaana na UD Songo,  leo Jumamosi ya wiki hii ukiwa ni mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika nchini Msumbiji.

Uhuru alisema UD Songo inapocheza mechi za kimataifa huwa inapata sapoti kubwa kwa wananchi wote tofauti na ilivyo kwa Tanzania. “Simba inaenda kukutana na timu ambayo inakuwa na ushindani mkubwa ikiwa nyumbani na ukiangalia wanajitahidi sana kupata matokeo kutokana na sapoti ambayo wanapata kwa nchi kwenye michuano ya kimataifa.

 

“Hawa UD Songo ni timu inayomilikiwa na kampuni ya kuzalisha umeme ya Cahora Bassa HCB na ukiangalia uwanja wao unachukua mashabiki 2000 tu, lakini mechi hizi kama za Simba na za kimataifa kwa ujumla wanahama kwao na kwenda Beira ambako kuna uwanja mkubwa ilikupata mashabiki wengi.

 

Na hupata sapoti kubwa ya nchi. “Mara nyingi UD Songo hutumia wachezaji vijana na hawana zile fitna za nje uwanja,” alisema Uhuru.


Loading...

Toa comment