The House of Favourite Newspapers

Simba Yatakata Lindi, Yazidi Kujikita Kileleni 3-1

0

COME back ya kibabe unaweza kuiita hivyo, baada ya timu ya Simba kuutoka nyuma kufungwa bao moja kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3 -1 dhidi ya Namungo Fc ya Ruangwa Lindi, kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa leo   Mei, 29.

 

Namungo walianza vema mchezo huo na kufanikiwa kupachika goli kupitia kwa Nzigamasabo dakika ya  23’ na kwenda mapunziko wakiwa mbele.

Kipindi cha pili baada ya mabadilko kadhaa ya kuingia kwa Hassan Dilunga na Bernard Morrison, kulifanya Simba kuanza kushambulia kwa haraka zaidi na Chris Mugalu akisawazishia Simba dakika ya 78.

 

Baada ya hapo Simba ilicharuka nahodha John Bocco akapachika na la pili dakika ya 83’ na Morrison akafunga ukurasa kwa kufunga goli kali la kideoni akiwa katikati ya uwanja dakika 87.

 

Simba imefikisha alama 64 baada ya  michezo  26, Yanga nafasi ya  pili inashikiliwa na  Yanga wakiwa  alama 61, baada kushuka dimbani mara 29.

 

Leave A Reply