The House of Favourite Newspapers

Simba Yatumia Mbinu za Al Ahly Kuimaliza Vita

KOCHA Mkuu wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems ni kama amewamaliza wapinzani wake AS Vita, baada ya juzi kuangalia kwa mara ya pili video ya mchezo wa Al Ahly ya Misri dhidi ya Vita ambayo Wakongo hao walishinda bao 1-0.

 

Katika mchezo huo, Simba inahitaji kupata ushindi wa aina yoyote ili iweze kufuzu katika hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo mikubwa.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Aussems alisema kuwa walishindwa kuangalia mchezo huo kutokana na kuwa kwenye maandalizi ya mchezo wa Saoura uliochezwa Algeria, hivyo ilikuwa ngumu kwake na wachezaji kupata muda wa kuutazama.

Aussems alisema, baada ya kuukosa mchezo huo, yeye na wachezaji wake pamoja na benchi zima la ufundi wameangalia jana kwa umakini mkubwa ili kujua udhaifu wao na wachezaji wapi hatari wanaohitaji kuchungwa watakapokutana.

 

Aliongeza kuwa, baada ya kuutazama mchezo huo kambini Sea Scape Beach Hotel, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam atajua aingie uwanjani na mbinu zipi za ushindi katika mchezo huo.

 

“Kama ilivyokuwa kawaida yangu, mara nyingi kabla ya kukutana na timu pinzani ninapenda kuwaangalia wapinzani wangu kwa kuziangalia video za michezo yao ya mwisho kabla ya kukutana na sisi.

 

“Hivyo, jana (juzi) usiku baada ya wachezaji kupumzika kutokana na uchovu wa mazoezi, nilikutana na wachezaji pamoja na benchi langu la ufundi hotelini kwa kuangalia video yao ya mchezo na Al Ahly,” alisema Aussems.

Comments are closed.