The House of Favourite Newspapers

Mo Awamwagia Milioni 150 AS VITA WAFE TAIFA

WACHEZAJI wa Simba sasa washindwe wenyewe tu kwani kwa kufuru aliyoitoa mwekezaji na mfanyabiashara maarufu, Mohammed Dewji ‘Mo’ ni ya kujipinda kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mechi ya leo dhidi ya AS Vita ya DR Congo.

 

Simba inacheza mchezo muhimu leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa kwani inahitaji ushindi wa lazima ili iweze kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Kutokana na ugumu huo, kumekuwa na ahadi mbalimbali kwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo lakini kubwa zaidi ni ile aliyoitoa Mo. Chanzo makini cha habari kimeliambia Championi Jumamosi kuwa, Mo Dewji, amewaahidi wachezaji na benchi la ufundi kuwa, endapo wataifunga AS Vita na kufanikiwa kuendelea katika hatua ya robo fainali, basi atawapatia kitita cha shilingi milioni 150 wagawane.

“Nilichokisikia kambini tangu jana (juzi Alhamisi) ni kwamba bosi Mo, ameahidi kutoa milioni 150, endapo tutafanikiwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo, jambo ambalo kiukweli limeongeza sana hamasa kwa upande wetu kama wachezaji.

 

“Hakuna mtu ambaye kesho (leo) ataingia uwanjani bila kuwa na hamu ya kumaliza mchezo akiwa na uhakika wa kuingiza fedha nzuri kama hiyo, ingawa hata bila fedha ya ziada bado mchezo wenyewe ni muhimu sana kwetu.

 

“Hakuna anayemhofi a Vita wala anayewaza mchezo na matokeo ya awali zaidi ya kuwazia ushindi tu hiyo kesho (leo),” kilisema chanzo hicho cha kuaminika kutoka ndani ya uongozi wa Simba.

 

Alipotafutwa Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema: “Hadi sasa sijapata taarifa kuhusu fedha hizo za ahadi, nachojua tangu tumeanza michuano hii kulikuwa na utaratiibu wa bonasi na upo tu tangu tuingie kwenye mihuano hii.

Musa Mateja, Dar es Salaam

Comments are closed.