The House of Favourite Newspapers

Simba Yavunja Mkataba Na Kocha Robertinho, Seleman Matola Atapewa Mikoba

0

Klabu ya Simba Sc imefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na kocha wao raia wa Brazil, Roberto Oliviera (Robertinho) siku ya leo Novemba 7, 2023 na kuvunja mkataba na kocha wa viungo, Corneille Hategekimana.

Taarifa iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula imeeleza kuwa katika kipindi cha mpito, Simba itakuwa chini ya Kicha Daniel Cadena akisaidiwa na Seleman Matola.

“Uongozi wa Klabu ya Simba unawashukuru makocha hawa kwa mchango wao ndani ya klabu yetu na inawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya,” imesomeka taarifa hiyo.

Leave A Reply