The House of Favourite Newspapers

Simulizi ya jina la Yao Ming inashangaza

0

YaoMingonoffense2NEW YORK, Marekani

WACHEZAJI kutoka nje ya Marekani wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali kutokana na mabadiliko ya tamaduni, lakini tukio la mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu katika Ligi ya NBA, Yao Ming aliyekuwa akiichezea Houston Rockets linachekesha.

Mkongwe huyo raia wa China, anasema kuwa licha ya kucheza katika ligi hiyo kwa muda mrefu, wachezaji wenzake walisababisha watu wamuite jina ambalo kiuhalisia hakuzoea kulitumia lakini akalazimika kukubali kutokana na kuwa muoga na mwenye aibu kuwaambia kuwa

 wanakosea.

“Nilipoingia kwenye ligi, Steve (Francis) alikuwa mtu wa kwanza kunisalimia, akanikumbatia kwa nguvu tofauti na nilivyozoea, baada ya hapo akaanza kuniita kwa jina la Yao ambalo ni la baba yangu. Kule kwetu (China) jina la mzazi huwa linaanza mwanzo kisha linafuatia la kwako.

“Nyumbani kwetu na hata marafiki zangu wote walifahamu kuwa mimi naitwa Ming na siyo Yao. Nilipoanza kuitwa Yao hata marafiki na ndugu zangu walishangaa lakini sikuweza kuwarekebisha wachezaji wenzangu kwa kuwa nilikuwa nina aibu.”

Leave A Reply