The House of Favourite Newspapers

SIMULIZI YA KUSISIMUA: THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)-24

0

MTUNZI: Hashim Aziz (Hashpower)

0719401968

ILIPOISHIA:

Kiukweli bado nilikuwa na hofu kubwa mno ndani ya moyo wangu, kumbukumbu za tukio lililotokea zilikuwa zikiendelea kujirudia kwenye kichwa changu, ikafika mahali kichwa kikawa ni kama kinataka kuchanganyikiwa.

“Vipi mdogo wangu, hebu twende huku,” alisema Bonta baada ya kuniona nasuasua pale juu nikiwa hata sielewi nini cha kufanya.

SASA ENDELEA…

“Piga msumari kwanza mambo mengine yote yatakaa freshi,” alisema huku akitoa msokoto wa bangi, akauwasha na kuvuta mafunda kadhaa, akanipa. Nilishindwa kukataa, kimsingi sikuwa nimewahi kuvuta bangi hata siku moja lakini kwa hali niliyokuwa nayo kwa wakati huo, niliona labda inaweza kunisaidia.

Nilivuta funda la kwanza, Bonta akawa ananitazama usoni, akanielekeza jinsi ya kumeza moshi. Nilipojaribu, moshi ulinipalia na kusababisha nikohoe sana, watu wote wakawa wanacheka kwa nguvu.

Nilipotulia, nilijaribu tena, nikavuta na kumeza kiasi kikubwa cha moshi, sikukohoa tena! Nikarudia tena na tena, nikaanza kuhisi kama kichwa chote kimekufa ganzi.

Bonta alikuwa akinisemesha lakini nilikuwa nikimsikia kwa mbali sana, ile hofu iliyokuwa imetanda kwenye kichwa changu ikayeyuka na nikaanza kujihisi kama raha fulani hivi ambayo ilinifanya nitamani kucheka.

Basi nilijiinamia palepale huku nikiwa natabasamu mwenyewe, Bonta akawa anacheka sana na kunipigapiga mgongoni.

“Shushia na hii,” alisema huku akichukua ule msokoto mkononi mwangu maana niliikuwa nimeushika tu ukiendelea kuisha, akanipa kichupa kilichokuwa na pombe kali, nikafungua kifuniko na kupiga funda moja.

Kila kitu kilibadilika, sikukumbuka tena chochote kilichotokea, nikawa najihisi nina raha kubwa sana ndani ya moyo wangu. Hata sijui tuliondokaje pale baadaye nilishtukia tu tukiwa ndani ya teksi na Bonta huku nikijihisi usingizi mzito sana.

Alinipeleka mpaka Sinza, akahakikisha naingia ndani na kufunga milango yote kisha akaniambia sitakiwi kutoka kwenda mbali biola kumpa taarifa. Kwa jinsi nilivyokuwa najisikia, nilienda kujitupa kwenye kochi, nikawasha redio na kufungulia sauti ya juu, usingizi mzito ukanipitia.

Nilipokuja kuzinduka, ilikuwa ni majira ya kama saa nne hivi za usiku, kichwa kilikuwa kinanigonga kwelikweli, nikaamka na kwenda kupunguza sauti ya redio, nikaingia bafuni kwenda kuoga kwani tangu nimerudi, sikupata hata muda wa kujimwagia maji.

Nilioga na kurudi kwenye friji, nikachukua chupa kubwa ya maji na kunywa kwa wingi maan animewahi kusikia kwamba maji ni dawa nzuri ya kichwa.

Baada ya kumaliza kunywa maji, nilianza kuhisi njaa kali sana, nikarudi chumbani na kubadilisha nguo, nikachukua noti mbili za shilingi elfu kumikumi na kabla sijatoka, nilichukua ile suruali niliyokuwa nimeivaa wakati natoka kazini, maburungutu yangu mawili ya noti mpyampya yalikuwepo.

Niliyatoa na kuyahifadhi chini ya godoro nilikokuwa nimeweka zile hela zangu nyingine, hata sikutaka kuhesabu kwa muda huo, nikavaa vizuri na kutoka kwa lengo la kwenda kununua chakula. Nilipakumbuka pale Cheers nilipopelekwa na Bonta, nikaamua kwenda kwa sababu nilikipenda chakula chake.

Nilipofika tu, wale wahudumu walinikumbuka, basi wakaja kunisalimu kwa bashasha huku wakikumbushia vituko vyango nilivyovifanya siku ile nikiwa nimelewa. Basi niliagiza chakula na kwa sababu ya kukwepa mazoea, sikutaka kukaa pale badala yake nikawaambia wanifungie.

“Najua umechoka sana, unaonaje leo ikienda kukuburudisha? Siku ile ulinikimbia lakini leo wala hujalewa! Nakupenda mwenzio,” alisema yule mhudumu ambaye nilikuwa nimekaa naye siku ile.

Kutokana na jinsi nilivyokuwa najisikia ndani ya moyo wangu, niliona kama nikiwa peke yangu naweza hata nisipate usingizi usiku kucha kutokana na hofu, sijui nilipata wapi ujasiri wa kumkubalia, nikamwambia tuondoke pamoja.

“Ngoja basi niage kwanza, kanisubiri kwenye Bajaj,” aliniambia huku akinikumbatia na kunibusu. Nilitoka na kwenda kwenye ile Bajaj niliyokuja nayo ambayo bado ilikuwa ikinisubiri. Dakika chache baadaye, yule msichana akiwa ameshabadilisha nguo za kazi, alikuja mbiombio mpaka pale.

Kidogo nimsahau kwa jinsi alivyokuwa amebadilika, kigauni kifupi alichokuwa amevaa, kilimfanya aonekane mrembo kwelikweli, basi akaingia kwenye Bajaj na kunibusu.

“Yaani huwezi kujua furaha niliyonayo ndani ya moyo wangu,” aliniambia huku akisaidia kubeba chakula, tukaondoka na Bajaj mpaka pale nilipokuwa naishi. Moyoni nilikuwa bado sijui nini kitaenda kutokea kule ndani kwa sababu kama nilivyowahi kueleza, pamoja na ujanja wangu wote sikuwa namjua mwanamke.

Basi tulipofika, nilimlipa dereva Bajaj fedha zake, kisha nikafungua mlango na kumkaribisha mgeni wangu.

“Unaishi na nani kwani?”

“Naishi na wazazi wangu sema wamesafiri kwa hiyo niko peke yangu,” nilimwambia, akawa anashangaa huku na kule. Aliniambia kwamba naishi maisha mazuri sana, nikawa namkwepesha kwenye hoja yake kwa kumwambia kwamba sifa hizo wanatakiwa kupewa wazazi wangu.

“Mh! Mbona humu ndani hakuna dalili kama unaishi na wazazi wako?” aliniuliza wakati akinisaidia kuandaa chakula, nikawa naendelea kumzuga. Sijui kwa nini sikutaka ajue kama naishi peke yangu!

Basi aliniandalia kila kitu kwa uchangamfu kisha tukakaa na kuanza kula. Yeye hakuwa akila bali alikuwa akiniandalia kila kitu, alinitolea mifupa kwenye nyama na wakati mwingine akawa ananilisha.

“Ujue mimi nakupenda sana, tangu siku ile nimekuona nimejikuta tu nikikupenda.”

‘Tangu lini muuza baa akampenda mwanaume?” nilimuuliza swali ambalo lilionesha kumuumiza sana moyo wake.

“Sijapenda kuwa muuza baa, ni maisha tu ndiyo yamefanya nikawa hivi. Nilikuwa na ndito nyingi maishani mwangu lakini zote zimeyeyuka!” alisema kwa huzuni huku machozi yakianza kumlengalenga.

Nilijilaumu kwa kauli yangu ile kwa sababu siku zote nilikuwa naamini kwamba wauza baa wote, ni wanawake ambao hawajatulia, hawawezi kuwa na uhusiano na mwanaume mmoja na kwao pesa ndiyo kila kitu.

“Kwa hiyo unafikiria na mimi labda huwa najiuza au kwako nimefuata pesa, kwa nini lakini unanifikiria hivyo,” aliniambia baada ya kumaliza kuondoa vyombo nilivyolia, nikamjibu kwa kifupi kwamba naomba anisamehe kama nimemhisi vibaya.

“Vyovyote utakavyonielewa, kama utaniona mimi ni malaya sijatulia, sawa! Ila nataka tu ujue kwamba nakupenda sana,” alisema huku akifanya kitendo ambacho sikutegemea kama atakifanya. Aliinama kidogo, akavua kufuli lake na kulitupa pembeni, akanisogelea pale kwenye kochi nilipokuwa nimejilaza kichovu. Hata sikupata muda wa kutafakari, akanivamia mwilini na kugusanisha ndimi zetu, kwa mara ya kwanza nikapata msisimko ambao sijawahi kuupata.

Sijui alitumia ujanja gani, nilishtukia tu mkono wake mmoja ukiwa umeshapenya na kuingia kwenye himaya ya ‘mkuu wa kaya’ na kumkamata, nikapatwa na mshtuko usioelezeka, mapigo ya moyo yakawa yananienda mbio kuliko kawaida.

“Tulia basi jamani, mbona unakuwa hivyo,” aliniambia baada ya kuona nimepoteza kabisa utulivu, nilikuwa nahangaika nikiwa hata sijui nataka kufanya nini, kimsingi nilipatwa na msisimko wa ajabu sana. Nilijitahidi kutulia kama alivyonielekeza lakini haikuwa kazi nyepesi.

Alichokifanya, alianza kunitoa magwanda mwilini mwangu, moja baada ya jingine mpaka alipomalizia la mwisho kabisa, na yeye akafanya hivyohivyo! Muda mfupi baadaye, tulikuwa saresare maua.

Aliniongoza nini cha kufanya na muda mfupi baadaye, tulikuwa tukiogelea kwenye bahari ya huba yenye kina kirefu.

Haukupita muda mrefu, nikaanza kutokewa na hali ambayo hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kunitokea, nguvu za mwili zikaongezeka na kunifanya na mimi niongeze kasi ya mchezo, sekunde chache baadaye tayari nilikuwa nimeshakwea kwenye kilele cha mlima mrefu kuliko yote barani Afrika, Mlima Kilimanjaro.

“Ndiyo mara yako ya kwanza eeh?” aliniuliza swali ambalo nilishindwa kulijibu zaidi ya kukwepesha macho yangu kwa aibu. Niliinuka na kwenda bafuni, nikajimwagia maji ambapo angalau akili zilirudi mahali pake, nilipotoka naye alienda kuoga na kurudi pale kitandani.

Kwa mara ya kwanza nilielewa maana ya mapenzi! Ile hofu niliyokuwa nayo ndani ya moyo wangu iliyeyuka na nikajikuta nikitamani kurudia tena na tena sanaa ile ya kikubwa, naye akawa ananipa ushirikiano wa kutosha na kunielekeza nini cha kufanya.

Mpaka tunakuja kulala, ilikuwa ni karibu saa nane za usiku, nikapitiwa na usingizi mzito kiasi kwamba sikuelewa tena kilichoendelea mpaka nilipokuja kuzinduka kukiwa kumeshapambazuka.

Je, nini kitafuatia? Usikose kesho hapahapa! Unaweza pia kusoma au kusikiliza hadithi nyingine kwa kuingia: www.simulizizamajonzi7113.blogspot.com ,  Facebook: Simulizi za Majonzi au Youtube: Hashpower Online. Usisahau kulike, share na ku-subscribe.

 

 

Leave A Reply