The House of Favourite Newspapers

Sina Doa: Ya Amber Rutty, Wema Yalishanitokea

MKALI wa Ngoma ya Ugwadu, Mary Mramba ‘Sina Doa’ amefungukia video chafu zilizovuja hivi karibuni za staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu na video vixen, Amber Rutty kuwa hata yeye yalishamtokea na kupita.

 

Akizungumza mbili tatu na Showbiz, Sina Doa ambaye alikuwa video vixen kwenye video kibao za Kibongo ikiwemo Rimoti ya Izzo B pamoja na Mwaka wa Roho Mbaya wa Nay wa Mitego alisema, aliumia sana video zake za faragha zilipovuja lakini mwisho wa siku yaliisha.

“Katika maisha kuna mapito mengi sana, haya wanayopitia sasa hivi Wema na Amber Rutty yalinitokea hivyohivyo, zilivuja nikawa nanyooshewa vidole kila ninapopita lakini nashukuru yaliisha wakasahau na sasa hivi nadunda tu,” alisema Sina Doa aliyewahi kubamba pia na Ngoma ya Hannah Montana.

Comments are closed.