The House of Favourite Newspapers

Singida Yamuuza Rasmi Kutinyu mil. 45 Azam FC

Mshambuliaji raia wa Zimba­bwe, Tafadzwa Kutinyu.

SINGIDA United rasmi imemuuza kiungo wake mshambuliaji raia wa Zimba­bwe, Tafadzwa Kutinyu dola 20, 0000 (sawa na shilingi milioni 45) kwenda Azam FC iliyokuwa inamuwania.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache ku­wepo na taarifa za kiungo huyo kuwaniwa na Simba ambayo ilikuwa inamuwinda vikali kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chao.

 

Kutinyu ni mchezaji wa pili kutua Azam baada ya hivi karibuni kufanikisha usajili wa mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma.

Kwa mujibu wa taarifa am­bazo Championi Jumatano inazo, kiungo huyo anatua kuichezea Azam akisaini mkata­ba wa miaka miwili.

 

“Kutinyu rasmi ni mchezaji wa Azam, hiyo ni baada ya kufi­kia makubaliano mazuri kati ya Singida na Azam yenyewe ambayo imekubali kununua mkataba wake wa mwaka mmoja alioubakisha.

 

“Ni kiasi cha dola 20,000 ambacho kimetosha Singida kumuachia kiungo huyo na ku­saini Azam na usajili huo tuna­ufanya kwa ajili ya msimu ujao ambao tumepanga kuchukua ubingwa,”alisema mtoa taarifa huyo kutoka Azam.

 

Alipotafutwa Meneja wa Azam, Philip Alando kuzungumzia hilo, simu yake ya mkononi iliita bila ya mafanikio, lakini hivi karibuni alitamba kufanya usajili mkubwa wa kutikisa ndani ya siku mbili kwa maana ya juzi na jana.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Comments are closed.