The House of Favourite Newspapers

Sinon Institute Of Education: Taasisi Inayoongoza Kwa Utoaji Wa Elimu

0

Hapa Kazi Tu na Tanzania ya Viwanda ndiyo kauli mbiu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na katika kumuunga mkono kiongozi huyo wa nchi, Taasisi ya Sinon Institute of Education, inatoa mafunzo yanayoweza kumfanya mhitimu akapata ajira kirahisi kwenye viwanda mbalimbali nchini.

Taasisi hiyo inatajwa kuwa kisima cha maarifa kutokana na jinsi inavyoweza kumuandaa mwanafunzi, kuanzia ngazi ya chini kabisa na kumfanya awe na thamani kubwa kwenye soko la ajira nchini.

 

Sinon Institute of Education iliyosajiliwa na serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatoa elimu kuanzia masomo ya elimu ya awali, msingi, sekondari, vyuo vya ualimu na mafunzo ya ufundi studi (TTC na VTC) ambayo yanawajengea wahitimu uwezo wa kujiajiri au kuajiriwa kwa maendeleo ya taifa.

Taasisi zilizopo chini ya Sinon Institute of Education ni pamoja na Healsun Pre and Primary School iliyopo jijini Arusha ambayo inatoa elimu kuanzia ‘baby class’, ‘middle class’, pre unit na darasa la kwanza hadi la saba.

Healsun inatoa nafasi kwa wanafunzi wa kutwa sambamba na wale wa bweni, kwa ada nafuu kabisa ya shilingi 480,000 kwa wanafunzi wa kutwa na shilingi 1,200,000 kwa wale wa bweni ambapo mzazi anarahishiwa ulipaji wa ada ambapo anaweza kulipa kidogokidogo kwa awamu nne.

 

Taasisi nyingine ni Healsun Technical Secondary School iliyopo jijini Arusha ambayo ni shule ya sekondari ya ufundi, inayotoa elimu kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne pamoja na ufundi.

Mbali na kupata elimu ya sekondari, lakini pia mwanafunzi atapata fursa adhimu ya kusoma Civil Engineering na Electrical Engineering kwa ada nafuu kabisa ya shilingi 1,540,000 ambayo mzazi anaweza kulipa kidogokidogo kwa awamu nne.

Sinon Teachers College iliyopo Sekei jijini Arusha ikiwa na tawi jingine lililopo Kimara Temboni jijini Dar es Salaam, ni taasisi nyingine iliyopo chini ya Sinon Institute of Education, ambayo ni inatoa mafunzo ya ualimu na ufundi stadi.

Kozi zinazotolewa na Sinon Teachers College ni ualimu wa awali (early childhood), ualimu wa msingi daraja la tatu (grade 3A) na diploma ya ualimu wa sekondari.

Taasisi nyingine ni Sinon Vocational Training College (Sinon VTC) inayotoa kozi za hotel management, tourism and tour guide, food production, cookery and bakery, food and beverage service and sales, kozi za uhazili (full secretarial stage I, II and III) na usimamizi wa biashara (business administration).

Kozi nyingine zinazotolewa na Sinon VTC ni computer courses, Information and Communication Technology (ICT), computer servicing and maintenance, kozi ya ufundi umeme (electrical insulation), hotel housekeeping and laundry pamoja na Computer Essentials Microsoft Operation.

Kwa wanafunzi wote, chuo kinawatafutia ‘fields’ kwenye ofisi mbalimbali, mahoteli sambamba na kwenye mbuga za wanyama kwa wanafunzi wanaosomea utalii.

Nafasi za hostel na chakula zinapatikana kwa bei nafuu kabisa na mzazi anaweza kuwa analipa ada kidogokidogo kwa awamu.

Namna ya kuwasiliana nao, fika kwenye ofisi na shule zao zilizopo Kimara Temboni karibu na shule ya msingi Kimara B kwa jijini Dar es Salaam au Sekei, Mount Meru karibu na Shule ya Msingi Sekei jijini Arusha.

Shule za Sinon za elimu ya awali, msingi na sekondari ya ufundi zipo Murieti Terati kwa Mromboo, jirani na Barabara ya East Africa (Bypass) jijini Arusha.

Unaweza kupakua fomu za kujiunga na masomo ya awali, msingi, sekondari na chuo kupitia website ya taasisi hiyo ambayo ni www.sieco.ac.tz au fika katika ofisi zao.

Kwa mawasiliano zaidi, unaweza kupiga simu namba 0754 681 720 au 0767 001 136, barua pepe (email), [email protected] au wafollow instagram kupitia Healsunschool &Sinon Institute na Facebook; Sinon Institute.

Leave A Reply