The House of Favourite Newspapers

SIRI YA ROSA REE KUTOBOA NI HII

Rosary Robert

MWANAMUZIKI Rosary Robert, ambaye anafanya vizuri kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva na Afrika kwa sasa na Wimbo wa Way Up aliomshirikisha Emtee wa Afrika Kusini, amefunguka kuwa bila kujiamini na kusimamia kile anachokiamini asingetoboa.

Akipiga stori na Showbiz Xtra, Rosa Ree alifunguka kuwa muda mwingi huko nyuma watu walikuwa wanamwambia kwamba anajifanya mnyamwezi kwa soko la Bongo hawezi kufika popote, lakini hakuwasikiliza kwa sababu alikuwa anawaza kwenda kimataifa.

“Nisingejiamini na kusimamia kile nilichokiamini kiukweli nisingefika mahali nilipo leo, siku zote nilikuwa ninatazama soko la kimataifa, kwa hiyo hata maneno ya kunikatisha tamaa sikupenda kabisa kuyapa nafasi,” alisema Rosa Ree.

BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.