The House of Favourite Newspapers

Sister Fay Aichokonoa Serikali

Faidha Omary ‘Sister Fay’

LICHA ya baadhi ya wasanii kufungiwa nyimbo na wengine kutofanya sanaa kutokana na kwenda kinyume na maadili, msanii wa filamu na muziki, Faidha Omary ‘Sister Fay’ anaonekana kuichokonoa serikali baada ya kueleza kuwa haachi kukaa nusu utupu kwani ndiyo asili ya Waafrika.

 

Akichonga na Za Motomoto News, Fay alisema kuwa, hawezi kuacha kujiachia mitandaoni nusu utupu kwa kuwa asili ya Waafrika ni kwamba zamani za mababu walikuwa wanajifunga kipande cha ngozi kiunoni na kifuani hadi pale wazungu walipoanza kuleta nguo hivyo haoni ajabu au tatizo la kukaa nusu utupu.

 

“Nashangaa sana tukikatazwa eti kukaa uchi wakati ndiyo asili yetu Waafrika kwani zamani mababu na mabibi zetu walikuwa hawavai nguo, bali walijifunga kipande cha ngozi kufunika maungo nyeti tu na sehemu nyingine za mwili zilikuwa zikiwa wazi. Kiukweli siwezi kuacha kukaa nusu utupu maana ndiyo ninapenda hivyo,” alisema Fay.

Comments are closed.