The House of Favourite Newspapers

Sister Fay, kiben’ten wake Wabwagana

BAADA ya penzi lao kutikisa mwaka jana, msanii wa Muziki Bongo Fleva, Fatuma Omari, ‘Sister Fay’ anadaiwa kutemana na kiben’ten wake Elias Shayo ‘Holly Star’.

Kwa mujibu wa chanzo, kwa sasa wawili hao hawapo pamoja na ndiyo maana hata kwenye mitandao ya kijamii kila mmoja amefuta picha za mwenzake.

 

“Ukiingia Instagram wamefutiana picha, kila mmoja ameamua kugeukia maisha yake. Hawaishi pamoja kama mume na mke walivyokuwa,” kilisema chanzo.
Za Motomoto ilimvutia waya Sister Fay ili aeleze kiundani juu ya madai hayo ambapo alipopatikana alikanusha.

 

“Jamani hatujaachana ni kwamba pale tulipokuwa tunaishi tumehama, tumehamia sehemu nyingine halafu kuhusu hizo picha zangu kufutwa mtandaoni, nilichukua simu yake nikazifuta picha zangu na kwenye simu yangu nikafuta zake,” alisema Sister Fay na kuongeza:

 

“Tumefanya hivyo kwa sababu sasa hivi nimeamua kufanya kazi za kijamii maana mambo ya mapenzi hatuhitaji tena kuyaweka mtandaoni, ila kwa sasa sijapata usajili wangu ndio maana nipo nafanya kazi na Flora Nitetee kwa ajili ya kusaidia jamii.”

 

NEEMA ADRIAN

Comments are closed.