The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI FEBR 13: PUNDA Walivyomponza MWIGULU, Asimulia Alivyotaka KUFA! – VIDEO

Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba amenusurika kifo baada ya ajali ya gari kutokea hii leo maeneo ya Migori mkoani Iringa akiwa njiani akitokea Iringa kuelekea Singida kisha kukimbizwa hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo Dodoma kwa matibabu zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Benjamin Mkapa alipolazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu, Mwigulu amesema alipata ajali baada ya gari lake kugonga punda waliokuwa wanakatisha barabara. Mwigulu amesema kuwa ghafla alisikia kishindo kikubwa kilichoashiria kuwa wamepata ajali kisha akaona Moshi unaoashiria gari kutaka kulipuka ambapo wasamalia wema walifika mapema kuwaokoa na kuwakimbiza hospitalini.

Akizungumzia tukio hilo Mkurugenzi wa hospitali ya Benjamin Mkapa, Dk, Alphonce Chandika amesema kuwa Mbunge huyo alifikishwa hospitalini hapo majira ya saa 3:30 asubuhi na kupatiwa huduma ya awali pamoja na vipimo.

Dk, Chandika amesema Mwigulu alikuwa analalamika maumivu makali kwenye maeneo ya kifua, nyonga na kwenye mguu ambapo walilazimika kumfanyia vipimo vya CT Scan, Ultrasound na X ray vilivyoonyesha hapakuwa na mfupa iliovunjika.

Comments are closed.