The House of Favourite Newspapers

SISTER P AIBULUWA TENA

Happy Pela ‘Sister P’

MKONGWE kwenye gemu la Bongo Fleva, Happy Pela ‘Sister P’ ameibuliwa upya kwenye muziki na mwanadada Matata ambaye ameamua kumsimamia ili aonyesha kipaji chake cha kuchana alichokuwa nacho tangu zamani. 

 

 Akizungumza na Mikito Nusu Nusu, Sister P, anayetamba na Ngoma ya Tingisha alisema kuwa, kipaji anacho sana ila alikuwa hana mtu wa kumuinua na kumsimamisha hivyo anamshukuru sana Matata kwa kumfikisha alipo.

 

“Yaani naamini hata upoteeje Mungu anaweza kukuibua kivingine kabisa kama alivyomleta Matata, yaani hapa nilipo niko vizuri kabisa na hata kama nilipotea kwa kukosa muongozo sahihi huyu dada ameniinua vilivyo kabisa,” alisema Sister P ambaye kipindi cha nyuma alitamba na Ngoma ya Anakuja

Stori: Imelda Mtema

Comments are closed.