The House of Favourite Newspapers

Sistinho: Simba Day Iitwe Jina la “Dalali Simba Day” Kumheshimu Muasisi

0
Mchambuzi wa soka Sistinho

MCHAMBUZI wa soka kupitia vipindi vya michezo vya Global tv na +255 Global Radio, Sistinho, amesema ni wakati wa Simba kuweza kutoa heshima kwa muasisi wa wazo la Simba Day Hassan Dalali, aliyekua Mwenyekiti wa Simba SC muongo mmoja uliopita kwa kumpatia tuzo au kubatiza Tamasha hilo jina lake kama heshima.

 

“Ni wakati wa Simba SC kumpa heshima stahiki mzee Hassan Dalali ambaye aliasisi mawazo haya ya kuanzisha Tamasha maalum, mawazo ambayo yameweza kuigwa na timu mbalimbali kama Yanga SC, Azam FC na Singida Big Stars, ndio yeye alitoa kipindi timu ikiwa kwenye mazingira magumu kiuchumi kwa lengo la kuchangia mapato lakini sasa hivi yamekuja na taswira nyingi mpya kama kurudisha mpira kwa jamii na kadhalika” alisema Sistinho.

Sistinho amesema Tamsha la Simba Day inabidi lipewe jina la “Dalali Simba Day” kama sehemu ya kuenzi mchango wa Hassan Dalali katika Tamasha hilo

Mzee Hassan Dalali alibuni na kuasisi Tamasha la Simba Day kama sehemu ya kuchangisha fedha kwaajili ya kununua eneo la Bunju ambalo kwasasa Simba wamejenga viwanja viwili vya mazoezi.

Leave A Reply