The House of Favourite Newspapers

Siwema: Kuachwa Kulinipa Akili

0
Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa na Siwema Edson.

 

MZAZI mwenziye na mwanamuziki Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson amefunguka kuwa kama asingepitia misukosuko ya kimapenzi na mzazi mwenziye huyo mpaka kuachana basi asingepata akili ya kujibidiisha kibiashara.

 

Siwema mwenye makazi yake jijini Mwanza, alisema baada ya kupata misukosuko alitafakari na kuamua kupiga moyo konde na kusimama kama mwanamke ili afanye kitu ambacho kitamsimamisha na kuendelea na maisha yake.

 

“Unajua ukikumbwa na misukosuko hasa ya kimapenzi akili inatanuka, nilijiongeza haraka na leo hii nina duka langu kubwa la nguo hapa Mwanza na maisha yanaendelea, ningekaa kulilia mapenzi ningechemka,” alisema Siwema.

Leave A Reply