The House of Favourite Newspapers

SIWEMA: UTOTO ULINITOA KWENYE MSTARI!

MWANADADA mjasiriamali ambaye pia ni mzazi mwenza na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson amekiri kuwa, kipindi cha nyuma alipoteza muda mrefu kutokana na mambo ya kitoto aliyoyafanya yaliyomfanya apotee kwenye kusaka mafanikio ya haraka.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Siwema ambaye kwa sasa anamiliki duka kubwa la nguo jijini Mwanza, alisema kilichomsaidia ni kwamba alikubali aliyumbishwa na utoto pamoja na masuala ya mahusiano lakini alifanya maamuzi sahihi kuyapokea makosa yake na kuyarekebisha.

“Mimi nilichukua pale nipokosea kama changamoto na kufanyia kazi sikukata tamaa na kujiona mnyonge nilijisihahisha kisha nikasimama tena, ningekata tamaa sijui ningekuwa mgeni wa nani,” alisema Siwema ambaye kwa sasa ameshaachna na Nay, kila mtu ana maisha yake

Comments are closed.