The House of Favourite Newspapers

Sizonje Wimbo wa Mpoto Unaompasua Kichwa Magufuli

0

MAGUFULIIIANDREW CARLOS, Dar es Salaam

“SIZONJE namjua unataka nikwambie? Nitakwambia. Kuna sehemu uliimba vile vyumba vitatu visivyofunguka milango, sasa mimi nitakuonyesha funguo zake zilipo,” hayo ni maneno ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli akimwambia mkali wa mashairi ya kughani, Mrisho Mpoto.

    zizonjeRais Magufuli hakuishia hapo: “Kati ya nyimbo ambazo nazipenda ni wimbo wako huu mpya wa Sizonje kwangu ni kama wimbo wangu wa taifa, naupenda sana, ni wimbo ninaosikiliza mara kwa mara.”

Kauli hiyo, ilikuja mara baada ya kushuka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar alipokuwa akitokea Mwanza, ambapo alipokelewa na kikundi cha ngoma cha Mpoto na ndipo Magufuli alipopata nafasi ya kuzungumza kwa ufupi na msanii huyo.

Hiyo ni bahati ya kipekee kwa msanii kuzungumza na rais wa nchi na kupewa ujumbe huo.

Wimbo wa Sizonje umejaa mafumbo mengi kuanzia jina la wimbo hadi mashairi yake, inahitajika akili ya ziada kudadavua yale yanayoimbwa na Mpoto.

Binafsi nimekuchambulia baadhi ya mashairi ya wimbo huo ambao unapendwa na Rais Magufuli:

IMG-20160218-WA0004(KIITIKIO – BANANA ZORRO)

Sizonje hii ndio nyumba yetu

Milango ipo wanapita madirishani

Sizonje ndio nyumba yetu

 Milango ipo wanapita madirishani

Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu

Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu

(Mpoto anamueleza Sizonje kama ndiyo rais aangalie nchi yetu na apambane na wale wanaopita njia za panya kupata mafanikio wakati njia halali zipo)

IMG-20160218-WA0009[VESI 1 – MRISHO MPOTO]

Karibu sana Sizonje, hii ndo nyumba yetu

Tulipoficha mundu za kupondea wezi

Kwani, makaburi yaliofukuliwa lazima yazikwe upya?

Nyumba hii Sizonje ina vyumba vinne

Vitatu havifunguki, kimoja hakina mlango

Japokuwa kina watu ndani, na hawaongei Kiswahili

Wenyeji wanalala sebleni na walishazoea.

IMG-20160218-WA0005(Karibu rais, hii ndiyo nchi yetu yenye silaha za kupambana na ufisadi na umasikini. Makaburi amemaanisha uozo kwenye nyanja mbalimbali uliopo tangu zamani. Vyumba vitatu bado ni fumbo lakini chumba cha mwisho amemaanisha wahamiaji wanaoishi nchini na kuwanyima ajira wenyeji).

Sizonje kule tulipotoka panaitwa jikoni

 Huna haja ya kwenda kule, kumejaa mafundi wa kupika

Sasa hivi wanakupikia wewe ili ule ulale

Ukiamka muongee nini hasa ujio na dhima ya safari yako

Wanashangaa mbona ghafla

Samahani sana mgeni

Wapishi wameniomba kwamba

Nikuulize tena kwa kukuomba kwamba

Eti unapenda vya mafuta au vya nazi?

Wanataka kukuonyesha madoido katika mapishi yao Sizonje

IMG-20160218-WA0003

(Rais anaoneshwa wizara nyeti zilizopo ndani ya nchi, wapishi ni viongozi wanaoongoza wizara hizo ambao wao ndiyo wanajifanya wanajua mipango yote, wanakukaribisha kama unatka kuingia kwenye mfumo wao).

Sizonje chumba hiki naomba usiingie

Ukimaliza nitakwambia kwa nini

Kuna sauti inajirudia mara kwa mara

Na hapa mlangoni kulikuwa na picha mbili kubwa

Moja picha, nyingine mchoro wa picha wa kwanza

Ninachokumbuka iliwahi kuandikwa

“USIYEMTAKA KAJA”

Hatukuwahi kuelewa maana yake

Labda kwa sababu ya ujio wako unaweza kutusaidia

(Kuna watu ambao huwa

 hawaguswi kwa kuwa wao ndiyo wanaoshikilia mifumo, hivyo rais akitaka matatizo basi awaguse watu hao kwa ubaya, usiyemtaka kaja hapa anamaanisha wapo waliokuwa hawapendi awe rais lakini amekuwa).

[VESI 2 – MRISHO MPOTO]

Najua, wimbo mbaya haufai kubembelezea mtoto

Na kamwe mtoto hawezi kuungua

Kwa kiazi kilichokuwa kwenye kiganja cha mama yake mzazi

Njoo huku uone Sizonje

Si unajua, harufu ya uzazi haiishi mpaka mtoto akue?

(Anamaanisha rais hawezi kumaliza ufisadi na uzandiki kwa mara moja kwa kuwa hayo ndiyo maisha ya watu kadhaa)

Sawa, Sizonje, huu hapa ni ua

Lile pale ni shimo la taka

Na kile pale ni choo

Kinachotutisha na kutuogopesha zaidi

Wanaoishi humu ndani

 hawajawahi kutupa taka

Wala kwenda chooni

Kama ukiwa makini

Kwa nje utasikia sauti za makundi ya watu

Wengi ni vijana, wana bahasha za khaki mikononi

“KAMA HAMTUPI TAKA SHIMO HILI MLICHIMBA LA NINI?”

Lakini pia kwenye sauti zao, Sizonje

Kuna watoto, wazee na kina mama

Ukiunganisha sauti zao ndio unapata hizo kelele

Ninavyosikia, ila sina uhakika

Waliambiwa kihistoria nyumba hii ni ya kwao

Na wana haki ya kutupa taka na kutumia choo hiki

Sasa, njoo nikuonyeshe huku uchochoroni

Uone maajabu mengine ya nyumba hii

Sizonje, ukiona tembo anaringa

Ujue mvua zinakaribia

(Taka imetumika kama soko la ajira kwamba wenyeji hawapati ajira na ajira nyingi zimekuwa za kujuana. bahasha maana yake ni vyeti. Anauliza kama wanasoma ajira hawapati kwa nini walienda shule?)

Leave A Reply