The House of Favourite Newspapers

Skauti Tanzania Yagonga Miaka 100

0
Skauti Mkuu, Mwantum Bakari Mahiza

 

Chama cha Skauti Tanzania kinatarajiwa kuadhimisha miaka 100 ya uskauti tangu kuanzishwa kwake, maadhimisho yatakayofanyika kuanzia tarehe 21 hadi 29 Julai mwaka huu kwenye makao makuu ya nchi mjini Dodoma katika viunga vya Chuo Kikuu cha Dodoma.

 

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Skauti Mkuu, Mwantum Bakari Mahiza kuwa ufunguzi wa maadhimisho hayo utafanyika tarehe 26 Julai, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu Hassan.

 

 

Aidha Mahiza amesema kuwa maadhimisho hayo yatakayofungwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, yatawakutanisha skauti wapatao elfu nne kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

 

Mahiza amesema kuwa wanatarajia kupokea wageni mbalimbali kutoka nchi jirani, pamoja na bara la Ulaya na Asia.

 

Kauli mbiu ya maadhimisho ya skauti ni “Kuwajenga Vijana Kuwa Wazalendo na Kufanya Kazi kwa Bidii kwa Maendeleo ya Nchi”.

Chama cha Skauti kilianzishwa mwaka 1905 na badaye huko Uingereza na muasisi Lord Baden-Powell na kisha kiliingia Zanzibar na hatimaye Tanganyika mwaka 1917.

 

PICHA NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply