The House of Favourite Newspapers

SKENDO YA WOLPER KUMKUWADIA DOGO JANJA UWOYA APANIKI

KUNA mtu anateseka? Staa wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya, anadaiwa kupaniki ile mbaya kufuatia skendo mpya mjini kwamba, mwigizaji mwenzake, Jacqueline Wolper Massawe (pichani), ndiye aliyemkuwadia aliyekuwa mumewe, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ kwa mwanamke mwingine, Risasi Mchanganyiko limeng’atwa sikio.  

 

Habari zilizosambaa mitandaoni wikiendi iliyopita zilidadavua kwamba, kwa sasa Dogo Janja ana ‘kifaa’ kingine kipya ambaye ni mtoto mkali, mkazi wa jijini Arusha aliyetajwa kwa jina moja la Linna. Baada ya kusambaa kwa video na picha za Dogo Janja ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na Linna wakiwa kwenye mahaba mazito ndipo baadhi ya watu wakaibuka na kila mmoja kuanza kusema lake.

 

NUSANUSA YA RISASI

Katika nusanusa yake, Risasi Mchanganyiko lilitonywa kuwa, kwa sasa uhusiano wa Uwoya na Wolper hauko sawa. Kufuatia bango hilo kuwa na madai mazito ya Uwoya kupaniki huku Wolper akitajwatajwa ndipo gazeti hili likalazimika kusaka ubuyu kamili.

CHANZO CHATIRIRIKA

“Mmemuona huyo demu mpya wa Dogo Janja kutoka Arusha? Huyo demu amesababisha bonge la msala kati ya Uwoya na Wolper. “Zamani Uwoya alikuwa hana ushosti na Wolper, lakini hapo katikati mambo yalinoga kinoma na wakawa marafiki wa kufa na kuzikana.

 

“Ilifikia hatua hadi Wolper akawa ndiye mbunifu wa mavazi wa Uwoya ambaye mkwanja umemtembelea kama wote. “Huku na huku, wiki kadhaa zilizopita Uwoya alimwagana na Dogo Janja na kurushiana maneno ya kashfa mitandaoni.

 

WOLPER KIKULACHO?

“Katika kupitapita ndipo Uwoya akatonywa kuwa kikulacho ki nguoni mwake kwani Wolper ndiye aliyemtafutia Dogo Janja huyo demu wa Arusha. “Baada ya hapo unaambiwa Uwoya akawa amepaniki ile mbaya na mpaka sasa sina uhakika kama wanazungumza,” kilimwaga ubuyu chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa mastaa hao wa Bongo Muvi.

 

WOLPER, UWOYA WASAKWA

Kufuatia sekeseke hilo, Gazeti la Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Uwoya ili kujua kama anateseka, lakini lilipomkosa ndipo likamgeukia Wolper. Katika majibu yake kuhusu sakata hilo, Wolper alifunguka: “Kikubwa ninafurahi kwa sababu baada ya kupelekewa hiyo ishu, Irene (Uwoya) hakutaka kuamini kwani ananijua jinsi ninavyompenda na kumchukulia.

 

“Anajua siwezi kuwa snichi kwake kwani ninamchukulia kama ndugu yangu. “So hata alivyoambiwa alikuwa ndiye mtu wa kwanza kukataa mimi kufanya hivyo.

“Anajua mimi siwezi unafiki ndiyo maana hujawahi kuona nikimposti Dogo Janja (kwenye ukurasa wake wa Instagram) na huyo demu ambaye ni mdogo wangu (Linna) maana nitakuwa mchawi. Yaani mchawi kabisa.

 

Ni bora Dogo Janja na huyo demu wasingenificha kama wana uhusiano maana walikuwa wananificha, wangeniambia, ningeona kawaida tu maana Irene (Uwoya) na Linna siyo ndugu, siyo marafiki na mapenzi ni popote. Kwa nini nilete kipingamizi? Ila tu ile kunikatalia kuniambia ukweli wameniona mimi ni mchawi.

 

“Na mimi ninamlaumu Dogo Janja maana Dogo Janja hajui undugu wangu na Linna kwa hiyo ninahisi alitumia uanaume wake kuni-block (mtandaoni). “Mpaka hapa ninakuambia huyo mdogo wangu, Linna siyo mteja wangu tena na hana tena ukaribu na mimi tangu awe na Dogo Janja.

DOGO JANJA MCHAWI?

“Sasa nikisema Dogo Janja mchawi nitakuwa mwongo? Mchawi ni mtu mharibifu. “Nilishangaa sana kusikia eti mimi ndiye nimemkuwadia wakati Dogo Janja nilikuwa ninamchukulia kama mwanangu na alikuwa shemeji yangu (kwa Uwoya). “Hiyo skendo ndiyo imenifanya niwakalie kimya Linna na Dogo Janja maana Dogo Janja alikuwa rafiki yangu kabla hata ya kuwa na Irene (Uwoya) na huyo aliyenaye ambaye ni mdogo wangu kabisa.

 

“Kinachoniuma sana ni huo uvumi ulivyotokea maana nilimuuliza huyo mdogo wangu (Linna) na Dogo Janja wakakataa katakata na meseji zao ninazo alafu eti leo hii ninaonekana…. (tusi) wakati Irene (Uwoya) ni rafiki yangu na ni mfanyakazi mwenzangu.” Hata hivyo, Wolper aliendelea kusisitiza kuwa pamoja na mambo hayo yaliyotokea, lakini urafiki wake na Uwoya upo palepale.

 

TULIKOTOKA

Uwoya na Wolper waliwahi kuwa kwenye bifu zito miaka ya nyuma, lakini baadaye waliyamaliza na kuwa marafiki wakubwa.

Comments are closed.