The House of Favourite Newspapers

Skudu Atoa Tamko Zito Akitokea Kwao Afrika Kusini

0
Staa wa kimataifa wa Yanga, Mahlatse Makudubela ‘Skudu ‘ akiongea baada ya kutua nchini akitokea kwao Afrika Kusini.

BAADA ya kutua nchini usiku wa kuamkia jana Jumamosi akitokea kwao Afrika Kusini alipokuwa akijiuguza majeraha, staa wa kimataifa wa Yanga, Mahlatse Makudubela ‘Skudu ‘ amesema anatamani kuona anaisaidia timu hiyo kushinda michezo iliyo mbele yao, huku akiweka wazi kwamba anataka kufunga mabao matano kwenye mchezo mmoja.

Skudu alipata majeraha hayo katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC, uliopigwa Agosti 9, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Majeraha hayo yamemfanya akose michezo minne.

Akizungumza na Spoti Xtra, Skudu alisema: “Nimefurahi kurejea tena Tanzania mara baada ya kupita muda mrefu tangu niliporejea nyumbani kujiuguza.

“Nimepokea taarifa nyingi za mashabiki kunitakia kheri kutokana na changamoto niliyokutana nayo, hili ni jambo ambalo limenitia moyo sana, lakini pia najivunia ubora wa timu yangu kwa kuwa na mwendelezo wa matokeo mazuri.

“Niliutazama mchezo ambao tulishinda mabao matano wiki iliyopita, ikanifanya niwe na hamu ya kuwa sehemu ya timu ya ushindi na ikiwezekana kufunga mabao matano peke yangu.”

STORI NA JOEL THOMAS

ALI KAMWE AMPIGIA SALUTI MAX – ”UKIKUTANA na SHABIKI wa KOLO USIBISHANE NAYE”…

Leave A Reply