The House of Favourite Newspapers

SOFIA MJEMA: TUPO KWENYE MCHAKATO WA KUWATENGENEZA KINA SAMATTA

0
Mheshimiwa Sophia Mjema akiwapa hamasa ya kimichezo vijana hao.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Sophia Mjema amesema wapo katika mchakato wa kutengeneza na kuibua vipaji lukuki hususani katika mpira wa miguu ili kutengeneza wachezaji wengi zaidi kutoka Tanzania watakaocheza ligi kubwa duniani kama Mbwana Samatta.

Ameyasema hayo leo Jumamosi katika fainali ya mpira wa miguu iliyozikutanisha timu za mpira wa miguu za chuo cha City College of Healthy Science na Kigamboni College Of Healthy Science na katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park  na City kuibuka washindi na kunyakua kombe hilo.

Aidha Mkurugenzi wa vyuo vya Afya vya City Colleges, Shabani Mwanga amesema kwa sasa wameanza na vyuo vya Afya na baadae wanamalengo ya kuanzisha mashindano yatakayohusisha vyuo vyote jijini Dar na baadae nchi nzima.

Mbali na kukuza vipaji amesema lengo lingine la mashindano hayo ni kuwajengea vijana, uzalendo wa nchi yao lakini pia afya bora.

 

HABARI/PICHA: WAANDISHI WETU/GPL 

Leave A Reply