The House of Favourite Newspapers

Solskjaer: Subirini Man United Itaamka

Ole Gunnar Solskjaer

KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, amesema kuwa anaamini wachezaji wake bado wanaweza kuamka na kufanya vizuri. United wamekuwa kwenye kiwango duni kwa sasa na wikiendi iliyopita walikutana na kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya West Ham.

 

Hata hivyo, kocha huyo amesema kuwa anaamini timu hiyo inaweza kufanya vizuri zaidi huko mbele kwa kuwa wachezaji wake wanaelekea kubadilika na kuwa bora kila siku.

Msimu uliopita Man United walimaliza kwenye nafasi ya sita na msimu huu wamepoteza wachezaji wao mahiri akiwemo mshambuliaji, Romelu Lukaku ambaye amekwenda Inter Milan.

 

Pia United wamempoteza mshambuliaji wao Alexis Sanchez ambaye naye amejiunga na Inter Milan kwa mkopo. “Kwangu naamini kuwa tupo kwenye mpito, kila siku tunaendelea na kasi ya kubadilisha baadhi ya vitu kuhakikisha wachezaji wanafanya vizuri.

 

“Kwangu kila mchezo nawaona wachezaji wangu wakifanya kile ambacho nawaeleza hivyo naamini kuwa huku mbele tutafanya vizuri,” alisema kocha huyo.

Comments are closed.