The House of Favourite Newspapers

Soudy Brown, Maua Sama Watiwa Mbaroni

MTANGAZAJI wa Clouds Media, Soudy Brown na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Maua Sama wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kosa la uharibifu wa mali.

 

Inadaiwa wawili hao walikamatwa jana kwa madai kuwa video yao imeonekana mitandaoni wakirusha pesa na kuzikanyaga huku wakicheza wimbo mpya wa ‘Iokote’ wa Maua Sama.

 

Imeelezwa pia kwamba baada ya kukamatwa, wawili hao walipelekwa Polisi Kinondoni lakini leo jioni wameshahamishiwa Kituo Kikuu cha polisi dar es Salaam (Central) kwa mahojiano zaidi.

Aidha, Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa watu hao.

Comments are closed.