The House of Favourite Newspapers

Ndugai: Ile Clip Imetengenezwa – Video

0

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema katika hotuba yake aliyoitoa hivi karibuni hakukuwa na hapakuwa na jambo la kukashifu wala kudharau juhudi za Serikali bali alikuwa anasisitiza ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali.

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 3, 2022 jijini Dodoma, Ndugai amesema; “Tarehe 26 December 2020 nilialikwa kwenye kikao fulani hao waliitwa mikalile ya wanyausi ni utamaduni wa wagogo na siku hiyo waliandaa vyakula vya asili ya Kigogo.

 

“Katika mazungumzo yale baadaye ikatengenezwa clip na baadhi ya watu wakakatakata mambo, wakawasilisha ujumbe nusu, ujumbe nusu ule umesababisha mjadala mkubwa katika nchi yetu, ambao mjadala umesababisha usumbufu wa hapa na pale” amesema Ndugai nakuongeza.

 

“Kwa hiyo niliona tukutane pamoja na mambo mengine niweke sawa jambo hilo lilivyokuwa, hapakuwa na lolote la kukashifu wala kudharau juhudi zozote za Serikali, tunahitaji Serikali na tunaiunga mkono. Katika mazungumzo yetu niliwataka wenzetu pamoja na mabo mengine tulipe kodi, ushuru na tozo mbalimbali huo ndio ulikuwa msisitizo wa hotuba yangu.

 

“Kwenye ujumbe wangu, hakukuwa na lolote la kudharau juhudi za serikali, serikali ni baba yetu na mama yetu, tunahitaji serikali na tunaiunga mkono na niliwataka wenzangu kujiimarisha kiuchumi, tulipe kodi na tozo, huo ndiyo ulikuwa msisitizo wa hotuba yangu.

Na huu ndio ulikuwa msisitizo wa hotuba yangu ili tuisaidie Serikali yetu na nchi kujitegemea zaidi. Na nikasema kwa nini sisi Bunge tulipitisha Tozo.

 

“Nikasema, endapo wenzetu mnaona wabunge tulifanya jambo baya kupitisha tozo, basi mtatuhukumu huko mbele. Sikumaanisha taasisi nyingine yoyote. Kufuatia hilo likajitokeza jambo la kama vile Spika anapinga mkopo wa Serikali wa tril 1.3, hilo binafsi limeniuma sana,” Spika Job Ndugai.

Leave A Reply