The House of Favourite Newspapers

SPIKA AMUANIKA LEMA: Unadaiwa MIL 419, Una STRESS, Ushugulikiwe – Video

Spika wa Bunge, Job Ndugai.

 

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai,  ameiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kumhoji Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema,  kuhusu uamuzi wake wa kuunga mkono kauli iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad kuwa bunge ni dhaifu, na wakati huohuo ameanika hadharani madeni ya mbunge huyo.

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema.

Akizungumza baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni leo,  Ndugai ametaka kamati hiyo ikutane leo  saa 8.00 mchana na kwamba ikiwezekana suala hilo kesho likamilike.

 

Akisisitiza kwamba haogopi kitu, Ndugai alisema: “Wanaofikiri sisi ni dhaifu, sisi sio dhaifu nishasema nikarudia na narudia tena, yeyote ambaye anaingia katika 18  yangu (eneo la madaraka yake) sisi tuko tayari na yeye.

 

“Mheshimiwa Lema atakwenda huko na kesho kunako majaliwa tutaifahamu hatma yake. Na mwingine anayejiona anaalikwa kabisa. Nataka sasa tuthibitishe kuwa Bunge hili la kumi na moja  kweli lina uongozi na tutathibitisha hatumuogopi yeyote.”

 

Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.

 

Katika hatua nyingine, Ndugai  amemfukuza bugeni, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko (Chadema) baada ya kupiga kelele kumpinga kiongozi huyo wakati akilitaja deni la Lema.

 

Ndugai alilitaja deni ambalo alisema Lema anadaiwa kutokana na mkopo, hatua ambayo Matiko aliipinga na hivyo kusababisha kuchukuliwa kwa hatua hiyo.

Comments are closed.