The House of Favourite Newspapers

Utata! Mrembo Mtanzania Aliyefia Uturuki, Inadaiwa Alifanya Surgery Akaoza – Video

0

Taarifa za kifo cha mrembo wa Kitanzania, Shufaa Kitwana almaarufu Shuu zinaendelea kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, ikidaiwa kwamba msichana huyo alifariki dunia akiwa nchini Uturuki.

Sababu za kifo cha Shuu nazo ni jambo lingine linalozidi kuzua utata ambapo Global TV imefunga safari mpaka nyumbani kwa mrembo huyo, Magomeni jijini Dar es Salaam uliko msiba wake.

Hata hivyo, ndugu wa Shuu wamegoma kutoa ushirikiano na hivyo kuwalazimu waandishi wetu kumtafuta Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa aliokuwa akiishi Shuu, ambako ndiko msiba ulipo.

Juma Salum ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mianzini, Kata ya Makurumla jijini Dar es Salaam ambapo alipohojiwa na Global TV, alikiri kupata taarifa za kifo cha Shuu ambaye amethibitisha kwamba alikuwa ni mwananchi wake na msiba upo kwenye eneo lake.

Kuhusu sababu za kifo chake, Mwenyekiti Salum ameeleza kwamba naye amesikia kwamba Shuu alifikwa na umauti akiwa nchini Uturuki kufanya upasuaji wa kurekebisha maumbile yake (sajari) ingawa amesema taarifa hizo siyo rasmi na wanaoweza kueleza vizuri chanzo cha kifo hicho ni familia ya marehemu.

Leave A Reply