The House of Favourite Newspapers

SportPesa, La Liga kuileta Sevilla kwa Simba

KAMPUNI ya Michezo ya Kubashiri ya SportPesa kwa kushirikiana na La Liga wanaileta Sevilla nchini Tanzania kwa ajili ya ziara ya kimichezo inayokwenda kwa jina la ‘SportPesa Laliga Challenge’.

 

SportPesa ambao ni washirika rasmi wa michezo ya kubashiri Afrika wa Ligi hiyo ya La Liga, wanawaleta nchini mabingwa hao mara tano wa Uefa Europa ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao ya msimu mpya wa 2019/2020.

 

Wakiwa nchini Tanzania, Sevilla ambao pia ni mabingwa mara moja wa La Liga, watacheza na moja yatimu washirika wa SportPesa kati ya Simba au Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas alisema; “SportPesa tunaendesha biashara yetu kwa kujihusisha na maendeleo ya soka kwenye nchi tunazoendesha shughulizetu kwa kushirikiana na wadau husika huku tukitumia washirika wetu wa kimataifa kuleta maendeleo hayo.”

 

“Mara ya mwisho dunia ilishuhudia klabu ya Everton ikitembelea Tanzania kwa mara ya kwanza na muitikio ulikuwa ni wa kipekee.

 

“Kutokana na SportPesa kuwa na ushirika na taasisi kubwa za soka duniani kama La Liga, tukaona basi ni vyema kuendeleza msisimko wa kimataifa kwa kuileta klabu ya Sevilla nchini Tanzania ambayo inacheza kwenye Ligi hiyo bora duniani.

 

“Lengo ni kuionyesha dunia kuwa Tanzania ni mahala sahihi kwa klabu kubwa duniani kuja kwa ajili ya ziara za maandalizi ya ligi bila kusahau kuvinadi vipaji adhimu vya soka vilivyosheheni,”

Comments are closed.