The House of Favourite Newspapers

SportPesa Yaendelea Kumwaga Zawadi


KAMPUNI ya SportPesa kwa kushirikiana na Kampuni ya Mtandao wa Simu za mkononi Tanzania, Tigo wanatoa zawadi za simu aina ya Samsung A10s kila siku, lakini mwisho wa mwezi huu Oktoba 30, mwaka huu, watawazawadia wateja wake gari mpya aina ya Renault Kwid kupitia promosheni ijulikanayo kama Faidika na Jero.

 

Mpaka sasa kupitia promosheni ya Faidika na Jero washindi 26 wameweza kupatikana ambapo kila mmoja ameondoka na zawadi ya simu.

Akizungumza mara baada ya droo ya wiki ya nne Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya alisema “kupitia droo za kila wiki hii tumeweza kupata washindi kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani , Tanga, Dodoma, Morogoro pamoja na Mbeya.

“Promosheni bado inaendelea na wiki ijayo tunatarajia kupata washindi wengine saba na washindi wa wiki hii watakabidhiwa simu zao siku hiyohiyo.”

“Washindi wa wiki hii ni pamoja na Gervas Chacha (Morogoro), Meshack Sanga (Mbeya), Brighton Mbundo     (Pwani ), na Hatibu Shabani, Enea Mtosa, Khalfan Juma na Ramadhani Tindwa (Dar).

 

Watumiaji wapya na endelevu wa mtandao wa Tigo wanapaswa kuweka pesa kwenye akaunti ya SportPesa kupitia huduma ya Tigopesa ili kuweza kushiriki na kujishindia zawadi kabambe kwa ajili yao.

Comments are closed.