The House of Favourite Newspapers
gunners X

SPORTPESA YAKABIDHI BAJAJ KWA MSHINDI

Tangu ameanza kucheza SportPesa haikuchukua muda mrefu mpaka pale alipotangazwa kuwa ni mshindi wa Shinda Zaidi na SportPesa na kufanikiwa kushinda Bajaj mpya  kutoka timu ya ushindi.

 Huyu ni Mgaya Hassan mshindi wa droo ya 43,  ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha SUA mkoani Morogoro, lakini ushindi wa Bajaj umemkuta akiwa jijini Dar es Salaam wakati akimalizia likizo yake kwa kaka yake. Timu Ya Ushindi haikutaka kumcheleweshea, ilimfuata mpaka Bunju, Dar es Salaam, nyumbani kwa kaka yake na kumkabidhi Bajaj hiyo.

Akikabidhiwa, Hassan alisema alianza kucheza SportPesa baada ya kusikia kwenye redio na televishen kuwa kuna Bajaj zinatolewa na yeye moja kwa moja akijisajili na kuanza kutupia ‘bashiri’ kwenye mechi  mbalimbali hatimaye kufanikiwa kushinda.

“Mimi ni mwanafunzi nasoma SUA Morogoro, taarifa hizi za ushindi zimenikuta hapa Dar es Salaam wakati nikiwa likizo, nimefurahi sana maana wakati nacheza wanafunzi wenzangu waliniambia mimi siwezi kushinda kwa sababu naweka pesa ndongondogo, waliamini kuwa wanaoshinda ni wale ambao hubashiri kwa pesa nyingi kumbe sivyo.  Kila mtu ana nafasi ya kushinda maana mimi nilikuwa nacheza kwa elfu mojamoja pekee, sasa nimeshinda najua  wakiniona ndipo wataamini, yaani nina furaha sana,” alisema Hassan

Aidha Hassan anasema Bajaj hiyo itamkomboa kutoka kwenye maisha ya sintofahamu na kuingia kwenye maisha mazuri huku akitegemea kipato kitakachopatikana kutokana nayo kumsaidia kwenye mahitaji yake ya chuoni na nyingine kuwawezesha ndugu zake ambao hawako vizuri kiuchumi.

“Daaah, maisha ya chuo ni magumu sana, unatoka chuo umechoka wakati mwingine huna pesa ya kula familia zetu nazo zinatoka katika mazingira ya kimaskini unajikuta huna cha kufanya lakini kwa ushindi huu wa Bajaj nitaweza kujikimu mimi mwenyewe maana kila siku nitakuwa na uhakika wa kupata chochote kutokana na Bajaj hii,” aliongeza Hassan.

Aliwaomba wanafunzi wenzake wa vyuoni na wale ambao wamefikisha umri wa miaka 18 na zaidi kucheza  SportPesa maana wanaweza  kujikuta wakiandika historia mpya kwenye maisha yao na kumudu gharama  ndogondogo zinazopatikana chuoni.

 

Comments are closed.