The House of Favourite Newspapers

SPOTI HAUSI: SIMBA DAY MATUKIO YALIYOJIRI/ USAJILI WA KASEJA

SIMBA jana imecheza na Timu ya Asante Kotoko ya kutoka Ghana ukiwa ni mchezo maalum wa kusherehekea Tamasha la Simba Day lililofanyika katika Uwanja wa Taiafa jijini Dar es Saalaam.

 

Simba imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Asante Kotoko ambapo mfungaji bao la simba ni Emmanuel Okwi aliyefunga dakika ya 76 kipindi cha pili, Adam Salamba akikosa penati dakika ya 83 kipindi cha pili.Kwa upande wa timu ya Asante Kotoko mfungaji wa bao hilo ni Obeid Owusu dakika ya 44 kipindi cha kwanza.

 

Simba Day ni mfululizo wa wiki ya Simba ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka na kilele chake kinakuwa tarehe 8, Agosti, 2018.

 

Siku hii Simba huitumia kwa kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wapya ambao wamesajiliwa na Simba kuelekea msimu mpya siku ambayo inafahamika kama Simba Day.

Comments are closed.