The House of Favourite Newspapers

SPOTI XTRA LAZIDI KUJIPANUA KWA WASOMAJI

Baadhi ya wafanyakazi wa Global wakiliuza gazeti la Spoti Xtra leo asubuhi.

KIKOSI kazi cha kampuni ya magazeti ya Global Publishers Ltd, leo kiliingia tena mitaani kulinadi gazeti la Spoti Xtra ambalo limeanza kutoka kila Alhamisi kuanzia wiki iliyopita. Kikosi kazi hicho kiligawanyika sehemu mbalimbali za Jiji la Dar  yakiwemo maeneo ya Makumbusho, Ubungo, Buguruni, Karume, Keko Tandika, Temeke na sehemu nyingine ambapo waliwauzia wasomaji gazeti hilo na kukusanya maoni yao.

Matukio katika Picha:

Msanifu kurasa wa Magazeti ya Global Publishers, Charles Mgela,  akimuonesha gazeti mpita njia eneo la Keko-Veta jijini Dar.

Mmoja wa maofisa wa Global akimuuzia gazeti msomaji eneo la Karume
Mwandishi wa Global, Zainab Malogo,  akiwa kazini maeneo ya Veta jijini Dar.
Meneja Usambazaji wa Global, Anthony Adam (mwenye kofia) akiwapa maelekezo wasomaji wa Tandika Sokoni.
Ofisa wa Global Publishers, Lawrence Kabende, akimuonyesha gazeti muuza kahawa wa Karume jijini Dar.
Mwandishi wa Global, Memorise Richard Mwamonje, akiwaeleza wasomaji jinsi wanavyoweza kunufaika kwa kununua gazeti la Spoti Xtra na kushiriki shindano lililomo.

PICHA: RICHARD BUKOS / GPL    

 

Comments are closed.