The House of Favourite Newspapers

BEN POL ATOBOA SIRI YAKE NA MONALISA

Image result for BEN POL
Benard Paul ‘Ben Pol’

STAA wa Muziki wa R&B, Benard Paul ‘Ben Pol’ ametoboa siri yake na mkongwe wa filamu Bongo, Yvonne Cherrie ‘Monalisa’ kwamba ni mwanamke namba moja kwake kuliko wasanii wote wa kike wa muziki na filamu Bongo.

Ben Pol ambaye ameachia Wimbo wa Ntala Nawe huku Monalisa akitumika kama video queen alisema kuwa, kwa muda mrefu Monalisa alikuwa akimhamasisha namna ambavyo anafanya kazi zake bila Skendo.

“Ananihamasisha kwa kweli kwa namna anavyojitunza, nimefarijika sana kugundua kwamba Monalisa pia anapenda muziki wangu same way mimi ninavyopenda kazi zake za filamu, nilikuwa na ndoto ya kufanya kazi naye siku moja, nashukuru Mungu leo imetimia, niwaombe mashabiki waingie kwa wingi kujionea kazi yangu mpya katika Mtandao wa Youtube niliyofanya naye inayoitwa Ntala Nawe,” alisema.

 

Ben Pol X Cedo – Ntala Nawe (Official Video)

Comments are closed.