Spoti Xtra Lazidi Kutikisa Kila Kona ya Dar – Pichaz

KIKOSI kazi cha wafanyakazi wa Global Publishers leo Alhamisi, Oktoba 11, 2018, kama kawaida yake, kimeingia tena mitaani kulinadi gazeti la Spoti Xtra linalotoka kila siku ya Alhamisi na Jumapili ambapo wasomaji walikuwa wakiligombea.

Kikosi hicho kilipita maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar kuanzia maeneo ya Mbezi Makonde, Mbezi Afrikana, Mbuyuni Salalsala hadi Tegeta ambapo wasomaji walionekana kulichangamkia kwa kulinunua.

Kufuati ya maombi ya muda mrefu ya wasomaji wetu, Gazeti Bora la Michezo nchini, Spoti Xtra, tangu Alhamisi, Septemba 20, 2018,  limeshaanza kutoka mtaani mara mbili kwa wiki, yaani kila Alhamisi na Jumapili kwa Tsh. 500 tu.

Spoti Xtra limesheheni takwimu za soka na michezo mbalimbali inayopendwa duniani, uchambuzi makini wa mechi na masuala ya michezo, bila kusahau ratiba na matokeo ya ligi zote kubwa duniani.

Aidha, Spoti Xtra limesheheni makala za kuvutia za michezo, stori za burudani na mastaa wa ndani na nje ya nchi.

Unaambiwa kwamba, Spoti Xtra linakupa uhondo zaidi kwa #Jero, pia linakupa fursa ya kushinda zawadi kibao zikiwemo jezi orijino za timu za Ulaya uzipendazo.

Wapenzi wa michezo wameshtuka, hawaendi kwingine, bali ni Spoti Xtra pekee, mwambie na mwenzako, #SpotiXtra ndo’ habari ya mjini.

Ndani yake kuna kuponi itakayokupa nafasi ya kushinda zawadi kibao, hujachelewa  #SpotiXtra #HapaNiUhondoTu kila Alhamisi na Jumapili.

Mbali na Spoti Xtra, pia Gazeti la Amani nalo lipo mtaani leo Alhamisi likiwa limesheheni habari kemkem za mastaa, burudani, kijamii, mikasa, simulizi na hadithi za kusisimua kwa Tsh. 800 tu.

Loading...

Toa comment