The House of Favourite Newspapers

Staa wa Bongo Movies Wolper Aokoka Kisirisiri, Abadilika Kimatendo

0
Mama P; ni staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper

Jacqueline Wolper au Mama P; ni staa wa Bongo Movies ambaye tangu atangaze kuwa anatamani kuokoka, amebadilika mno kimatendo.

 

Watu wa karibu wa Wolper wanadai kuwa, mama huyo wa watoto wawili ameokoka kisrisiri.

Wakati hayo yakisemwa na yeye akikiri kwamba, siyo yule wa zamani, pia Wolper anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na mpenzi wake wa muda mrefu ambaye pia ni baba watoto wake, Rich Mitindo.

 

Wolper ni mongoni mwa waigizaji wa Bongo Movies wanaoshabikiwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii ambaye ameendelea kupokea hongera zake baada ya kutangaza kwamba sasa ni mama wa watoto wawili hivyo ameachana na mambo ya kidunia.

 

Wolper anasema kuwa, amefikia wakati anahisi kwamba upako wa Mungu umetua kichwani mwake na anahisi kama ameitwa kulihubiri neno la Mwenyezi Mungu.

 

“Kiukweli nafsi yangu inanituma kumtumikia Mungu wangu; yaani nitoe ushuhuda na nimuimbie kwa sauti ya juu hadi wanyama wasikie; yaani nina hiyo roho na sijui imetoka wapi. Mungu tenda miujiza yako nikakutumikie wewe kuokoa vijana waliopotea,” alisema Wolper.

 

Wengi wa mashabiki wake wanafurahia hatua hiyo na kumpongeza kwamba kama kweli roho wa Mungu amemtuma basi asijaribu kukwepa kama Yonah kutoka biblia na ni sharti atii kile ambacho Mungu amemtuma kufanya.

Stori; Ijumaa Wikienda, Dar

XCLUSIVE: SALEH JEMBE Achambua, YANGA vs CLUB AFRICAIN, MBINU za KOCHA NABI, UBOVU wa YANGA ni HUU!

Leave A Reply