The House of Favourite Newspapers

Stella Joel Afagilia Studio ya Injili Kujengwa Arusha

0

stella-joel.jpgStori: mwandishi wetu

KATIBU wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Stella Joel amemuunga mkono mwimba Injili anayekuja kwa kasi nchini, Godwin Maimu ‘Nnyaka’ kujenga studio ya nyimbo hizo jijini Arusha akisema itachangia kukuza muziki huo Bongo.

godwin

Godwin Maimu ‘Nnyaka’

Stella aliiambia safu hii kuwa, Nnyaka ameonesha njia ya kupita kwa kuweka studio ya muziki wa Injili na pia kurekodi nyimbo zote zenye maadili ya taifa, hivyo kuwataka waimba Injili wa Kanda ya Kaskazini kwenda huko.

Kwa upande wake, Nnyaka alisema kwa kuanzia, kwenye studio hiyo amerekodi nyimbo zake tisa ambazo zinatamba kwenye vituo vya redio nchini.

“Mimi mwenyewe nimeweke mfano, nimerekodi nyimbo tisa katika Albamu ya Nimekusamehe. Hivyo, wasanii wote wanakaribishwa na wakitaka kujua studio ni bora, wasikilize nyimbo zangu kwenye redio,” alisema.

Leave A Reply