The House of Favourite Newspapers

Stephane Aziz Ki na Khalid Aucho Waliamsha Rwanda

0
Khalid Aucho

MAJINA ya mastaa watatu wa Yanga, Djigui Diarra, Stephane Aziz Ki na Khalid Aucho, ndio gumzo hivi sasa, wakisubiriwa kwa hamu kubwa nchini Rwanda kabla ya kikosi hicho hakijatua kwa ajili ya mchezo wa hatua ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Jumamosi ya wiki hii, Yanga inatarajiwa kucheza dhidi ya Al Merrikh kwenye Uwanja wa Kigali Pele nchini Rwanda kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa mujibu wa Mwandishi wa Habari za Michezo Rwanda, Kagabo Kagishaz, Aziz Ki na Aucho ndio gumzo, wakisubiriwa kwa hamu kubwa na Wanyarwanda.

Kagishaz aliongeza kuwa, pia mashabiki wa soka Rwanda wana hamu kubwa ya kumshuhudia kipa raia wa Mali, Djigui Diarra akiwa golini.

Aziz Ki

“Yanga ina wachezaji wengi wakubwa, lakini Jonas Mkude, Aziz Ki na Aucho ndio ambao wanapendwa zaidi Rwanda na wako na mvuto mkubwa kwa mashabiki hivi sasa hapa nchini.

“Lakini pia wanatamani sana kumuona golikipa Diara, ambaye katika msimu uliopita alifanya mengi makubwa katika Kombe la Shirikisho Afrika ikiwemo kubeba Tuzo ya Kipa Bora.

“Hapa kilichobaki ni wao tu kupambana uwanjani bila kuwadharau Al Merrikh, ambao hapo nyuma wameshafanikiwa kuvuka hatua hii na kufuzu mara tatu mfululizo kuanzia msimu wa 2020/21,” alisema Kagishaz.

STORI NA WILBERT MOLANDI

Leave A Reply