The House of Favourite Newspapers

Sterling Aaaga Rasmi Manchester City, Akwea Pipa Kuelekea Marekani Kujiunga na Chelsea

0
Ujumbe wa Raheem Sterling kwa mashabiki wa Manchester City

MCHEZAJI wa Manchester City na Timu ya Taifa ya Uingereza Raheem Sterling (27) ameandika ujumbe maalum wa kuwaaga mashabiki wa Manchester City akiwa anaelekea kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Chelsea ya hapo hapo Uingereza.

 

Katika ujumbe wake Sterling amewashukuru mashabiki na timu ya Manchester City pamoja na bechi la ufundi kwa ujumla kutokana na namna walivyokuwa naye katika nyakati nzuri na nyakati ngumu klabuni hapo.

Raheem Sterling anatarajia kujiunga na Chelsea kutokea Manchester City

Akiwa na Manchester City Raheem Sterling amefanikiwa kucheza jumla ya michezo 339 akifanikiwa kufunga jumla ya mabao 131 na akitoa pasi 95 za mabao huku akifanikiwa kutwaa mataji 10.

 

Taarifa zinadai tayari Sterling ameshasafiri kuelekea nchini Marekani ambako klabu ya Chelsea imeweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2022/2023

 

 

Leave A Reply