The House of Favourite Newspapers

STEVE NYERERE FUNGA ZIPU

STEVE Nyerere funga zipu kaka unaaibika’! Ndivyo walivyosikika baadhi ya mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva waliofurika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro usiku wa kuamkia Jumatatu iliyopita.

 

Aliyekuwa akiambiwa maneno hayo si mwingine bali ni mwigizaji maarufu wa vichekesho Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ baada ya kushangaza wengi kwa kupanda jukwaani kisha suruali kumvuka kwa staili ya mlegezo na kuonekana akiwa hajafunga zipu.

 

Tukio hilo la aina yake lilijiri usiku huo kwenye lile tamasha kabambe la Wasafi Festival lililokuwa kwenye mkoa huo wa tatu baada ya kung’oa nanga mjini Mtwara na Iringa.

RISASI LASHUHUDIA

Kituko hicho kilichoshuhudiwa na Risasi Jumamosi kiliibua mayowe ya aina yake huku Steve Nyerere akiwapotezea mashabiki hao na kuendelea kuwapandisha stejini mastaa wenzake wa Bongo Muvi, Aunt Ezekiel na Jacqueline Wolper.

 

WAKATI WA WOLPER

Katika tukio hilo, Steve Nyerere alimpandisha kwanza Aunt stejini ambapo kwa staa huyo hakukuwa na kelele kama ilivyotokea wakati alipompandisha Wolper. Akiwa stejini, baada ya kujitambulisha, Wolper aliyekuwa akishangiliwa kwa kuitwa shemeji huku akishinikizwa kumuita Harmonize, mrembo huyo aliomba ajitokeze mwanaume rijali kutoka Morogoro ili amtunuku kuwa mpenzi wake.

 

Kufuatia ombi lake hilo, alipanda jamaa mmoja ambaye alimpigia magoti Wolper na kumuomba amkubalie awe mpenzi wake, jambo ambalo Wolper alimwambia watakubaliana ilimradi awe na matunzo yaani ajue kutunza mwanamke kwani hakuna mwanamke au mwanaume mbaya duniani.

Wakati yote hayo yakiendelea, Steve Nyerere alikuwa amemsogelea Wolper kisha kumshika kwa nyuma kwenye sehemu ya kiuno au nyonga na hapo ndipo zipu hiyo ilipoonekana mubashara ikiwa wazi na kusambabisha mayowe huku mwanadada huyo akipewa lawama lukuki za kumkubalia jamaa huyo kumshika maeneo hayo hatarishi.

 

“We’ Steve Nyerere funga zipu kaka, kitendo cha kumshika tu Wolper tayari na zipu umefungua, kweli wewe hatari,” alisikika mmoja wa mashabiki hao. “Funga zipu wewe huyo ni shemeji yako kwa Harmonize kwani hujui hilo?” Alihoji shabiki mwingine akimtaka Steve Nyerere kutokuleta mambo ya Bongo Muvi stejini hapo.

 

Hata hivyo, Steve Nyerere alijishtukia na kuona aibu ambapo katika kuua so alijifanya kugeuka nyuma na kuwapa mgonjwa mashabiki kisha kuifunga zipu hiyo.

STEVE NYERERE ANASEMAJE?

Kufuatia tukio hilo, gazeti hili lilimvaa Steve Nyerere na kumhoji juu ya kituko hicho, lakini hakuwa tayari kueleza chochote zaidi ya kufunga zipu hiyo iliyokuwa wazi.

 

KIFUATACHO…

Baada ya tamasha hilo kufana vilivyo kwenye Mikoa ya Mtwara, Iringa na Morogoro, leo ni zamu ya Sumbawanga, Rukwa kisha Desemba 11, watakuwa visiwani Zanzibar, Desemba 15, Mwanza, Desemba 26, watakuwa Mombasa kisha Nairobi itakuwa Desemba 31.

UWOYA Kabanwa kuhusu DOGO JANJA, Sikia Alichojibu!

Comments are closed.