The House of Favourite Newspapers

Straika Mghana anukia Simba SC

0
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe.

SIMBA ipo mbioni kumleta nchini straika Mghana ambapo viongozi kadhaa wa timu hiyo wamethibitisha ishu hiyo lengo likiwa ni kuimarisha kikosi chao. Inaelezwa kuwa, Simba wameghairi kumleta Mzambia, Walter Bwalya kutokana na gharama zake kuwa kubwa, na sasa akili yao ipo kwa Mghana huyo ambaye hajatajwa.

Tayari uongozi umeshakubali kumpa mkataba Mghana huyo baada ya mmoja wa vigogo wa timu hiyo kuridhishwa na uwezo wake. Chanzo makini kutoka ndani ya Simba kimesema kuwa, kigogo huyo hivi karibuni alikwenda Ghana, akiwa huko alipata nafasi ya kumshuhudia mchezaji huyo kuanzia mazoezini mpaka katika mechi, na akamkubali.

“Kama utakumbuka, hivi karibuni Kotei (James) wakati anaoa,  kuna kiongozi mmoja alikwenda Ghana, hivyo akiwa huko alipata nafasi ya kukutana na mchezaji huyo na alipomuona mazoezini na kwenye mechi, akakubali uwezo wake, akatuma taarifa kwamba anafaa. “Aliambiwa kama kuna uwezekano amalizane naye kila kitu hukohuko, lakini ikaonekana kuna ugumu, hivyo tunasubiri akitua ndiyo apewe mkataba.

“Waliosababisha mpaka mchezaji huyo kupatikana ni wale Waghana, Agyei (Daniel) na Kotei, kwani ndiyo waliosema ni mchezaji mzuri na anafaa kuichezea Simba,” kilisema chanzo hicho. Championi Jumatano lilizungumza na kigogo huyo wa Simba aliyekwenda Ghana kuzungumza na straika huyo, ambapo alithibitisha kuwa taarifa hizo ni za kweli.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, alipotafutwa jana kuzungumzia ishu hiyo, hakupatikana.

STORI:MUSA MATEJA

Leave A Reply