The House of Favourite Newspapers

Straika Wa APR Afuata Saini Yanga

MPACHIKA mabao tegemeo wa Klabu ya APR ya Rwanda, Issa Bigirimana ‘Walcott’ amesema kuwa yupo tayari kutua nchini na kusaini mkataba wa kuichezea Yanga kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

 

Yanga hivi sasa ipo kwenye mi­pango ya kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao na kati ya safu ambayo inahitaji marekebisho ni safu ya ushambuliaji inayoan­damwa na wachezaji wengi maje­ruhi nao Amissi Tambwe na Donald Ngoma.

 

Walcott alikuwepo kwenye kikosi cha APR kilichotolewa na Yanga kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2016 kwa kufungwa mabao 2-1 na yeye alikuwa tishio kwenye safu ya ulinzi ya Wanajangwani.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi kutoka Rwanda, Walcott alisema yeye mkataba wake un­amalizika Julai 3, mwaka huu hivyo yupo tayari kujiunga na Yanga kama wana nia ya kumsajili kwa ajili ya msimu ujao.

Aliongeza kuwa, wapo wachezaji waliomvutia yeye kuja kucheza soka nchini hapa akiwemo kiungo mchezeshaji Mnyarwanda. Haruna Niyonzima anayeichezea Simba akitokea Yanga baada ya mkataba wake kumalizika msimu uliopita.

 

“Ni muda wangu muafaka ume­fika wa mimi kuondoka hapa Rwan­da na kuja kucheza soka la kulipwa Tanzania na nipo tayari kujiunga na timu itakayovutiwa na mimi ikiwemo Yanga ambayo nimepata taarifa za kuhitaji mshambuliaji.

 

“Pia, nipo tayari kuzichezea timu nyingine kama Simba, Singida na nyingine zozote kikubwa nitaanga­lia maslahi pekee yatakayonishawi­shi mimi kusaini.

 

“Mimi hadi hivi sasa nimefunga mabao saba na anayeongoza ana mabao 11 wakati ligi ikielekea ukin­goni,” alisema Walcott anayetumia miguu yote miwili katika kupiga mashuti.

Alipotafutwa Niyonzima kum­zungumzia mshambuliaji huyo alisema “Jamaa anajua. Ni mchezaji mzuri na ni kati ya washambuliaji wanaokuja kwa kasi nyumbani Rwanda.

Comments are closed.