The House of Favourite Newspapers

Studio Zimekuwa Dili

0
Dully Sykes

MAKALA: BONIPHACE NGUMIJE | UWAZI | SHOWBIZ

SUALA la wanamuziki Bongo kumiliki studio sikuhizi si geni kabisa. Tofauti na zamani walipokuwa ‘wanahustle’ kwenye studio za watu wasainishwe kwenye ‘lable’ ili kurekodi nyimbo zao ama kutakiwa kulipa pesa, siku hizi wengi wao wanamiliki studio zao wenyewe.

Barnaba

Jambo ambalo ni zuri kwenye muziki kwa sababu wanakuwa na uhuru wa kufanya wanachotaka na kuboresha zaidi kazi zao, katika muda wowote.

Juma Nature

Nafasi ambayo wengi wao hawakuwa wanaipata kwenye studio za watu, ambapo walitakiwa kulipia pesa na kupewa muda wa kurekodi, ukimalizika hakuna mjadala, watapewa walichokifanya ama kama kuna marekebisho yatafanyika kwa kuongeza pesa.

Nay wa Mitego

Hata hivyo mbali na studio hizo kuwasaidie wasanii wengi katika kufanya kazi zao wengi wanazitumia kama chanzo cha mapato yaani ni biashara zao za kuwaingizia mkwanja.

Prof. Jay

Ingawa wengi wao wamekuwa si wawazi katika hili kusema ni kiasi gani cha fedha wanatoza underground ama mastaa wanapokwenda kurekodi, lakini pia fedha kwa jumla wanazoingiza, ukweli ni kwamba zimegeuka kuwa dili.

Navy Kenzo

Ndiyo maana hawazifungi na wanamudu ghalama za uendeshaji pamoja na kulipa kodi za maeneo wanayofanyia kazi.

Hata hivyo wafuatano ni baadhi ya mastaa wanaomiliki studio Bongo na maeneo ambayo studio hizo zipo!  

Leave A Reply