The House of Favourite Newspapers

Mwenge wa Uhuru Wazindua Mirandi mbalimbali Kinondoni

0

MANISPA ya Halimashauri ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam umezindua miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo miradi ya ujenzi wa shule ya Msingi Ali Hapi iliyopo Bunju,Mradi wa ujenzi wa daraja lililojengwa na wananchi wa JWTZ lililopo Mbweni,mradi wa ujenzi wa wodi za wazazi kituo cha Afya Kijitonyama na miradi mingine.

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi leo amekabidhiwa Mwenge wa uhuru na DC Sofia Mjema mara baada ya  kumaliza ziara katika Wilaya ya Ilala.

Mara baada ya kukabidhiwa Mwenge huo katika halmashauri ya manispaa ya kinondoni ziara ya mwenge katika manispaa hiyo imeanza kwa kukagua miradi na kuweka mawe ya msingi katika miradi ambapo Mh. Hapi ameishukuru serikali ya awamu ya tano ya Dkt. John Pombe Magufuli.

Kituo kipya cha Polisi Mbweni  kimegharimu shilingi milioni 850 ambapo hadi sasa takribani milioni 600 zimeshatumika.

Mh. Hapi amesema kuwa kituo hicho ni cha pili kwa ukubwa ambapo  kituo cha kwanza kwa ukubwa ni Ostabey na kubainisha kuwa kimejengwa kwa msaada wa mchango wa wananchi.

Mchango wa ujenzi huo ni kutoka Kampuni ya Shubashi kwa shilingi milioni 400, TRA milioni 100, IPTL milioni 10 na Twiga cement ambayo imetoa cement 1000.

Aidha Hapi amesema kituo hicho ni rafiki kwa jamii na kuwa kitasaidia kuimarisha ulinzi hasa kwa wahalifu wanaofanya biashara kinyume na sheria.

Nae kiongozi wa mbio za Mwenge Amour Hamad Amour akiwa ziarani katika kiwanda cha Woiso OriginalProducts amempongeza mmiliki huyo kwa juhudi za Tanzania ya viwanda na kusema hiyo itasaidia vijana katika ajira na kujikwamua kiuchumi.

Amour amewataka watanzania kuthamini bidhaa za nchini na kuwaasa vijana kujiepusha na uvivu na badala yake wajenge tabia ya kufanya kazi kwa bidii ili kujikwamua kiuchumi.

Pamoja na hayo amewaomba wamiliki wa viwanda vidogo kulipa kodi kwa wakati ili kuleta maendeleo kwa serikali na kuhakikisha rushwa inapigwa vita katika maeneo ya kazi na kutoa ajira kulingana na uwezo wa mtu.

Aidha amesema Tanzania bila maambukizi ya Vvu inawezekana hivyo jamii ijilinde kwa pamoja ili ifikapo mwaka 2030 isiwe na maambukizi.

Mbali na hayo amesema ni vema jamii  kujikinga na kutibu malaria  mapema ili kuongeza nguvu kazi ya Taifa katika kufikia Tanzania ya Viwanda.

Leave A Reply