The House of Favourite Newspapers

Suge Knight Ategemea Magereza Kumruhusu Kwenda Kumzika Mamake

Suge Knight

PRODYUZA na mfanyabiashara mkubwa wa masuala ya muziki nchini Marekani, Suge  Knight, anategemea mamlaka za magereza zitamruhusu kwenda kumzika mama yake, Maxine Chatman,  ambaye amefariki jana katika hospitali moja huko Paramount, California.

Suge ambaye yuko rumande akikabiliwa na kesi ya mauaji, alimtembelea kwa siku mbili marehemu mama yake mwezi Aprili mwaka huu alikokuwa anatibiwa.

Mwanamke huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kupooza uliomkumba mwezi uliopita ambapo hali yake ilikuwa inazidi kuharibika kutokana pia na matatizo ya figo.

 Maxine Chatman akisaidiwa na nduguze wakati wa uhai wake.

Comments are closed.