The House of Favourite Newspapers

Supermoon: Mwezi Mkubwa Mwekundu Utaonekana Wapi?

0

MAPEMA tarehe 26 mwezi Mei utakuwa katika wakati maalum. Kupatwa kwa mwezi mwaka 2021 kunafanyika huku mwezi ukitarajiwa kuwa mkubwa na mwekundu.

 

Tunaelezea tukio hilo na pale ambapo matokeo yake yataonekana. Kupatwa kwa mwezi hutokea wakati dunia inapitia kati ya mwezi jua na kuweka kivuli katika mwezi.

 

Mwezi, Jua na dunia lazima ziwe katika mstari mmoja kwa tukio hilo kufanyika. Vilevile mwezi mkubwa na mwekundu hutokea wakati mwezi kamili au mpya unapokaribia njia ya mwezi duniani.

 

Hatua hiyo huufanya mwezi uonekane mkubwa. Mzunguko wa mwezi upo mviringo, na upande mmoja (apogee) uko takriban kilomita 50,000 zaidi kutoka kwa dunia kuliko ule mwingine (perigee). Hivyobasi mwezi unaojitokeza karibu na perigee unaitwa Mwezi mkubwa.

 

Tukio hili hujulikana pia kama “superluna ya maua” kwasababu hutokea wakati maua yanapochipuza katika chemchemi ya ulimwengu wa kaskazini.

 

Data ya mwezi mkubwa

Wakati wa kupatwa, Mwezi utaonekana kuwa mwekundu kwa sababu mwanga wa jua hautafikia Mwezi moja kwa moja, lakini sehemu ya nuru hiyo itachujwa na anga ya Dunia na rangi nyekundu na rangi ya machungwa itaonekana kwenye setilaiti yetu.

 

Tukio hilo la kushangaza linajulikana kama “mwezi wa damu. Mabadiliko haya ya rangi hayatokani na mabadiliko ya Mwezi wenyewe, lakini kwa sababu Mwezi utaelekea kwenye kivuli cha Dunia,” Patricia Skelton, mtaalam wa nyota katika Shirika la Royal Observatory huko Greenwich, alielezea Wanahabari.

 

“Anga ya Dunia huangaza nuru ya jua na kuufanya mwezi kuwa mwekundu.” Katika kielelezo hiki, ambacho sio cha kupima, unaweza kuona maeneo mawili ya kivuli ambacho Dunia hutoa wakati wa kupatwa kwa jua, umbra na penumbra.

 

Kupatwa kutaonekana wapi?

Kupatwa kwa mwezi Mei 26 kutachukua dakika 15 na kutaonekana katika maeneo ya Amerika ya Kusini na pwani ya magharibi ya Amerika Kaskazini. Pia kutaonekana kidogo katika sehemu za Amerika ya Kati na mashariki mwa Amerika Kusini.

 

Inaweza pia kuonekana katika sehemu ya mashariki mwa baadhi ya nchi za bara Asia, na eneo la Oceania. Hii ni tukio la kwanza la kupatwa kwa mwezi kati ya manne ambayo tutayaona 2021.

 

Mnamo Juni 10 kutakuwa na tukio jingine la kupatwa kwa jua . Kupatwa tena kwa mwezi kutafanyika mnamo Novemba 18 na tukio la mwisho litakuwa la kupatwa kwa jua mnamo Desemba 4.

 

Je ni salama kuutazama?

Huku matukio ya kupatwa kwa mwezi yakitajwa kuwa hatari kutazama moja kwa moja, mwangaza wa kupatwa kwa mwezi ni mdogo hivyobasi ni salama kutazama bila kutumia vifaa vyovyote.

 

Je ina muhimu gani?

Tukio hilo ni la mwisho kwa watazamaji wa anga nchini Uingereza kuona kupatwa kwa mwezi kwa kipindi cha muda mrefu hadi 2029- hali ya hewa itakaporuhusu.

Leave A Reply